Home DOKUMENTARI Sir Alex Ferguson awapotezea Arsenal

Sir Alex Ferguson awapotezea Arsenal

9539
0

Niliamka asubuhi ni Mapema ili kuandaa timu yangu. Nikapokea simu ya mtu ambaye wala sikumjua. Akanieleza kwamba kuna dili la kuifundisha Arsenal. Muongeaji wa kwenye simu alikuwa na haraka sana alinihitaji nisafiri mpaka London kesho yake. Niliporudi nyumbani sikutaka kumwelleza yeyote suala lile.

Hayo yalikuwa maneno ya Sir Alex Ferguson alipopokea dili la kuinoa Arsenal mwaka 1986.

Sir Alex Ferguson alieleza mnamo mwaka 2011 namna alivyokataa kujiunga na Arsenal.

Ferguson, alipata mafanikio makubwa sana akiwa na klabu ya Aberdeen. Alifutiliwa na maskauti wa klabu inayopatikana kaskazini mwa London ili kuchukua nafasi ya Don Howe majira ya joto 1986.

Ferguson wakati huo Ferguson alikuwa kocha mkuu wa Scotland iliyokuwa ikijiandaa na michuano ya kombe la dunia kule Mexico.

Anasema sababu kubwa ni maandalizi ya kombe la dunia ndiyo yaliyomfanya kuchelewa kujiunga na Arsenal.

“Nilipa dili la kuinoa Arsenal nilimtafuata Walter ambaye nilifanya nae kazi timu ya taifa ya Scotland tokea 1985 baada Jock Stein kufariki.

“Nilitaka kumshawishi tuondoke wote Scotland na kujiunga na Arsenal. Wakati huo tulikuwa tunaelekea kwenye mchezo kule Israel. Tulipofika Tel Aviv nikamuita chemba na kumweleza kwamba Arsenal wananihitaji”

Kumbe Smith alikuwa na makubaliano ya kwenda Ibrox, kumsaidia Graeme Souness. Wala hakuonesha shaka [Smith] akaniambia pale [Arsenal]? Nenda ile ni timu kubwa.

Nikamwambia kiroho safi nataka tuende wote. Nakuomba kubali kujiunga na mimi!!

“Smithi akanivunja moyo na kuharibu kila kitu baada ya kuniambia mimi naenda Rangers. Nilishtuka sana. Nikamuuliza tokea lini? Akaninijibu kwa kipindi kirefu nilikuwa na makubaliano nao lakini sikutaka kumwambia yeyote.

“Baadae nikagundua Graeme Souness na Walter walikuwa na ukaribu mkubwa ndio maana alipopewa dili la kuionoa Rangers alimuomba Swahiba wake huyo waongozane nae.

“Shida ya Arsenal walitaka jibu la haraka. Sikuweza kuwajibu kwa haraka kwa sababu akili yangu yote ilikuwa inawaza kuhusu Mexico. Arsenal wakashindwa kuvumilia na mwisho wa siku dili likafa. Walter akatimkia Rangers mimi nikajiunga Manchester United”

Ferguson anasema mafanikio aliyoyapata Aberdeen yalimfanya atafute changamoto nyingine na aliamini kuwa England ilikuwa sehemu sahihi kwa yeye kutafuta fursa.

“Nilipata kila kitu nilichohitaji pale Aberdeen. Umri wangu pia uliruhusu. Mawazo ya kwenda England yakainiingia”

“Hata Rangers walikuja mwaka 1983 nikaaona sio vyema kwenda kwa wapinzani wangu. Tayari nilishajenga heshima kubwa klabuni Aberdeen. Kwenda Rangers ingekuwa usaliti. Nilikiwa na mahusiano mazuri na mwenyekiti Dick Donald, na makamu wake Chris Anderson, nikaona kwenda Rangers ingekuwa sawa kuwatukana.

“Hivyo nikaona bora niende England, nakumbuka Dick Donald aliniambia hakuna klabu itakayonifaa zaidi ya Manchester United. Ukweli nilipofika Manchester baada ya miezi 6 nilijiona nipo nyumbani”

Ferguson na Smith walikutana tena pale united mwaka 2004. Wakati huo Carlos Queiroz aliondoka United na kwenda Real Madrid lakini akarudi msimu uliofuata.

“Nilijua tu Carlos atarudi tu maana alikuwa na wakati mgumu sana pale Madrid,”

Imetafsiriwa na Privaldinho (Instagram)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here