Home Ligi LA LIGA SIO ZA KUKOSA: mechi za kukata na shoka

SIO ZA KUKOSA: mechi za kukata na shoka

9154
0

Bila shaka makocha wengi kwa sasa watakuwa wanakenua. Wachezaji wachache sana tumepokea taarifa za majeruhi. Naam. Kipute cha ulaya kimerudi sasa. Ule mchezo wa kujaribisha mapanga kwenye migomba umekwisha. Wikiendi hii kutakuwepo na vipute vya kukata na shoka.

Baadhi tu hizi hapa.

March 31: Everton vs Man City


Mechi hii ni mechi muhimu sana kwa Man City na ni mechi muhimu sana kwa Mashabiki wa Man United. Kama City atashinda mchezo huu basi mchezo unaofuata wa Man United dhidi ya Man City itakuwa mechi ya kukabidhiwa ubingwa. ni fedheha kubwa ndani ya Manchester Derby, Man united kutoa nafasi ya bingwa ambae ni mpinzani wake mkubwa. Safari ya kwenda kutawazwa mabingwa kwenye Derby yao itafanikishwa na karamu ya ushindi watakayopata Goodison Park.
March 31: Sevilla vs Barcelona


Barcelona wana tatizo la majeruhi kwa sasa. Wasiwasi mkubwa ni suala la Messi kama atakuwa fiti au lah. Sergio Busquets bado atakuwa nje ya uwanja kwa matatizo ya mguu. Blaugrana watasafiri kwenda mpaka kunako Estadio Ramón Sánchez Pizjuán. Sevilla wametoka kupata ushindi mnono kabisa dhidi ya Man United katika uga wa Old Trafford hivyo watakuwa na hamasa kubwa sana.

March 31: Juventus vs Milan

AC Milan wametoka kuadhibiwa na Arsenal nje ndani lakini vijana hawa wa Rossoneri watahitaji kupigania nafasi ya 4 kupata nafasi ya kushiriki tena michuano ya UEFA mwakani. Sala za Kocha mkuu wa Napoli Maurizzio Sarri zitakuwa upande wa Gattuso atakapohitaji Ac Milan kushinda au Kutoka Sare. Juventus wameipita Napoli Alama mbili tu hivyo watahitaji kwenda juzi zaidi ili kujihakikishia nafasi ya kutwaa ubingwa.

March 31: Bayern Munich vs Dortmund 

Ni mchezo wa mahasimu wa muda mrefu. Mchezo huu hautoi uelekeo wa ubingwa ila watacheza kwa ajili ya heshima za pande zote mbili. Dotmund atapigania nafasi ya pili ili kumpa Schakle nafasi ngumu ya kumfikia.

March 31: LA Galaxy vs Los Angeles FC

Utakuwa mchezo wa kwanza kwa Zlatan Ibrahimovic akiwa na La Galaxy. Mashabiki wanaomkubali Zlatan watatazamia Derby hii kubwa Marekani. Sio mchezo wa kuvutia sana duniani lakini ujio wa Zlatan utabadilisha upepo wa watu wa Sweden

March: Arsenal vs Stoke City

Wazee wa unga unga mwana. Mchezo mwingine wa kukata na shoka. Arsenal hawajui kesho kuhusu UEFA. wapo wapo tu. Mchezo muhimu kabisa kwenye kumalizia ligi. Piga ua lazima Arsenal washinde mchezo huu. Stoke ni moja ya timu ngumu. Tuone itakuwaje
Sunday, April 1: Chelsea vs Tottenham

Kama kuna mechi itamtoa Conte kijasho chembamba basi ndio hii. Manara angekuwa msemaji wa FA basi angesema This is London derby. Hii ni ile mechi ya unatoa au hutoi. Tottenham wapo juu kwa tofauti ya alama 5 dhidi ya Chelsea. Kama Chelsea atapoteza mchezo huu nina uhakika wasilimia 90 kuwa hawatashiriki UEFA mwakani. Kama Tott atashinda basi atakuwa ameweka gepu la alama 8.

Imeandaliwa na Privaldinho (Instagram)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here