Home Kitaifa Singida United yaomba kubadilishiwa uwanja

Singida United yaomba kubadilishiwa uwanja

3182
0

Singida United imethibitisha kuomba mechi yao ya Azam Sports Federation Cup ambayo itachezwa mwishoni mwa wiki hii dhidi ya Coastal Union uchezwe kwenye uwanja wa Azam Complex badala ya Namfua mkoani Singida.

Mkurugenzi wa Singida United Festo Sanga amethibisha na kutaja sababu za kuomba mchezo wao uchezwe uwanja wa Azam Complex.

“Ni kweli Singida United imeomba uwanja wa Azam Complex kwa ajili ya mechi ya tarehe 23 mwezi huu dhidi ya Coastal Union mechi ya kombe la Federation Cup.”

“Sababu zilizopelekea tuombe uwanja wa Azam Complex ni kwamba tarehe 20 timu yetu imecheza mchezo wa ligi Mtwara dhidi ya Ndanda lakini tarehe 23 inatakiwa icheze Namfua Singida mchezo wa Federation dhidi ya Coastal.”

“Kwa mazingira hayo inakuwa vigumu kwa sababu umbali wa kutoka Mtwara hadi Singida ni takribani siku mbili maana yake timu ikitoka tarehe 21 itafika tarehe 22 tumeona tutakuwa hatujajipanga na wachezaji watakuwa wamechoka kuelekea mechi ya tarehe 23.”

“Tumewaomba TFF watupangie uwanja mwingine na wao wameonesha ushirikiano tumepata uwanja wa Azam Complex ambapo tarehe 23 saa 1:00 usiku tutacheza dhidi ya Coastal Union.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here