Home Kitaifa Simba yamuweka mguu ndani mguu nje kocha Azam

Simba yamuweka mguu ndani mguu nje kocha Azam

3578
0

Kuna tetesi kwamba huenda kocha wa Azam FC Hans van Pluijm akatimuliwa katika klabu hiyo kutokana na mwendelezo wa matokeo mabaya ya hivi karibuni kwenye mechi za ligi kuu Tanzania bara.

Inaelezwa kuwa, hatua za kumfukuza kocha huyo zilianza baada ya Azam kulazimisha sare ya 1-1 na Coastal Union kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga lakini uongozi wa klabu hiyo ukaamua kuvuta subira kuona hali itakuwaje kwenye mchezo dhidi ya Simba.

Baada ya kipigo cha jana (Azam FC 1-3 Simba) huenda Babu Hans akapigwa chini wakati wowote.

Jana akiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari baada ya mchezo, aliulizwa kuhusu kuwepo tetesi za yeye kutimuliwa lakini Hans alisema swali hilo ni vizuri kama wataulizwa viongozi wa Azam.

“Hilo swali unatakiwa kuuliza uongozi, makocha wanaajiriwa na kufukuzwa mimi na wachezaji tunajaribu kufanya kila niwezalo ili tupate matokeo mazuri”-Hans van Pluijm.

Baada ya kupoteza mchezo wa jana dhidi ya Simba, Azam inakua imecheza mechi 5 mfululizo za ligi bila ushindi. Kati ya mechi hizo tano, imepoteza mechi mbili na kutoka sare mechi 3.

Matokeo ya Azam katika mechi 5 zilizopita (Ligi Kuu Tanzania Bara)

Azam 1-1 Alliance
Lipuli 1-1 Azam
Tanzania Prisons 1-0 Azam
Coastal Union 1-1 Azam
Azam 1-3 Simba

Hadi sasa Azam ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania bara ikiwa na alama 50 baada ya michezo 25 wakati Yanga (wanaoongoza ligi) wana pointi 61 wakiwa wamecheza mechi 25 sawa na Azam.
Nyuma ya Azam ipo Simba (nafasi ya tatu) imecheza mechi 18 ina alama 45.

Azam ilishinda ubingwa wa ligi kuu kwa mara ya kwanza na pekee msimu wa 2013/14 ambapo msimu huo alianza kocha Stewart Hall baadaye akamalizia Joseph Omog tangu hapo Azam imeajiri makocha na kuwafukuza bila kushinda taji la ligi kuu wengi wakiishia kushinda Kagame Cup na Mapinduzi Cup.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here