Home Kitaifa Nyota watatu Simba OUT Arusha

Nyota watatu Simba OUT Arusha

3847
0

African Lyon leo itakuwa mwenyeji kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abei Arusha kucheza na Simba mechi ya ligi kuu Tanzania bara mchezo utakaochezwa kuanzia saa 10:00 jioni.

Simba imekuwa na rekodi nzuri inapocheza dhidi ya Afeican Lyon, katika mechi 12 iliyopita Simba imeshinda michezo 10, sare 1 na African Lyon imeshinda mchezo mmoja.

Mechi ya leo inachezwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid ambao hauruhusu sana aina ya uchezaji wa Simba (pasi fupifupi) nadhani tayari benchi la ufundi la Simba linafahamu hilo.

African Lyon inapaswa kuanza kuvuna pointi kwa sababu hadi sasa wapo katika nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa ligi. Simba inaingia kwenye mchezo huu ikiwa inapewa nafasi kubwa ya kushinda ili kutetea ubingwa wake lakini African Lyon yenyewe inahitaji kubaki kwenye ligi kwa ajili ya msimu ujao.

Simba itawakosa wachezaji wake watatu Emmanuel Okwi, Juuko Murshid na Meddie Kagere kwenye mchezo wa leo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya African Lyon.

Kagere alisafiri na timu kwenda Arusha japo hatakuwa seemu ya kikosi cha mchezo wa leo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here