Home Kimataifa Simba: Ujuaji umeponza wengi

Simba: Ujuaji umeponza wengi

4121
0

Mnakumbuka mwaka jana wakati Pep anachinjwa na Liverpool klabu bingwa? Unajua ni kwanini? Kwa sababu ya ujuaji. Unakumbuka wakati Simba anapigwa 5 pale Kinshasa, unajua ni kwanini? ujuaji.

Wale Al Ahly ni miamba ya soka wa Afrika. Simba haipaswi kwenda pale kichwa kichwa. Inapaswa ichukua tahadhari kubwa sana. Kuna mambo kadhaa ambayo yatawaponza aidha Simba au Al Ahly.

Al ahly washajua Simba ni dhaifu baada ya kuogeshwa 5-0 , Hivyo wanajua Simba ni Underdog. Kitakachowaponza ni kudharau na kucheza kwa kujiamini bila kujilinda.


Timu zilizofungwa magoli mengi mpaka sasa klabu bingwa 2019

1. Simba – Magoli – 5⃣
2. ASEC – Magoli – 5⃣
3. Wydad – Magoli – 4⃣
4. Saoura – Magoli – 4⃣
5. Horoya – Magoli – 4⃣


Kucheza kwa nidhamu kutaifaidisha Simba alama. Wao wakicheza kwa kushambulia sana, Simba inapaswa icheze kwa kujihami. Siku zote mtu anayekushambulia sana huwa anajisahau kujilinda, tukumbuke alichowafanya Fernando Torres Barcelona pale pale Camp Nou.

Kama Simba itacheza kwa kufunguka na kujaribu kumiliki uwanja hapa napata ukakasi hasa ukitazamia Al ahly wapo kwao. Ni ngumu sana mchezaji kutulia akiwa anazomewa hasa kwa wachezaji wetu ambao hawajawahi kucheza mechi nyingi zenye changamoto kubwa ya mashabiki zaidi ya 10,000 wanaowazomea.


Shirikisho la soka Misri lietangaza kuwa mashabiki watakaoruhusiwa kwenye mchezo kati ya Al Ahly na Mnyama ni 10,000 tu


Al Ahly wakiwa nyumbani ni wakorofi kuanzia ndani na nje ya uwanja. Wachezaji wake ni ngumu sana kukubali kugawana alama.

Ni heri Simba wawaache Al Ahly wacheze wao kwa ujuaji kisha nafasi za Simba watazipata kupitia makosa yao.

Ulinzi imara unakupatia matokeo popote pale lakini kucheza kwa fujo bila nidhamu ya ulinzi hasa kwa kumdharau mpinzani wako utaambilia aibu.

Al Ahly katika ligi yao msimu huu ndio klabu iliyoruhusu magoli machache zaidi (12) katika michezo 16.

Aussems kwanza aheshimu uwezo wa Al ahly pia atumie uzoefu alio nao kujaribu mbinu mbadala ya kujua ni kwa namna gani wachezaji wake watacheza bila presha.

Siwezi kumfundisha kitu Aussems maaa ni kocha mwenye uzeofu wa miaka 30 ya uzoefu wa soka la Europe, Asia, na Africa. Aussems’ anamiliki leseni ya UEFA (UEFA Pro License) mimia hata ukocha ligi ya mbuzi sijawahi. Aliweza kuisaidia Nepal, kupanda viwango vya FIFA kwa alama 11 kutoka #192 to #181.

Aussems aliisaidia Benin kufuzu mashindano ya mwaka CAN 2008 kule Ghana, pia alifanya hivyo mwaka 2010 kule Angola. Baadae akaisaidia timu ya vijana ya U19 & U16 kushiriki michuano ya African Cup CAF mwaka 2009. Aliweza kuisaidia Benin kwenye viwango vya FIFA kuruka nafasi 55 , kutoka #114 mwaka 2006, hadi nafasi ya #59 mwaka 2009. Lakini CV yake haitufanyi tuwe vipofu wa madhaifu ya Simba. Yanaonekana wazi na yanashaurika labda tu mwenyewe ajitie ujuaji kwa sababu tu ana CV kubwa.

Kaunta ataki itawafaa sana Simba hasa ukiangalia Kagere ni kiberenge, Okwi ni kiberenge. Lakini mechi kama hii unahitaji mtu kama Dilunga ambaye anafanya maamuzi ya haraka.


Al Ahly wamefungwa mechi 4 kati ya 80 za nyumbani katika michuano ya klabu bingwa tokea 2005

❌2016: 1 – 2 ASEC Mimosas
❌2015: 3 – 4 Orlando Pirates
❌2014: 2 – 3 Al Ahly Benghazi
❌2013: 0 – 3 Orlando Pirates


Hawa akina Chama mechi za ugenini anacheza kama yupo nyumbani. Ni fundi sana lakini katika mechi ambazo unahitaji mtu mwenye maamuzi ya haraka na ambaye hakai na mpira sana Chama hafai labda kama atacheza kama kiungo wa juu au mshambuliaji msaidizi na sio kiungo wa katikati.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here