Home Kimataifa Simba imeelekea Congo, Manara katoa neno

Simba imeelekea Congo, Manara katoa neno

4732
0

Klabu ya Simba imeondoka asubuhi ya leo kwenda jijini Kisnshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya AS Vita katika Kundi D la ligi ya mabingwa Afrika.

Afisa habari wa klabu ya Simba Haji Manara amesema timu yao imejipanga kupata matokeo mazuri kwa ajili ya nchi na kwa maslahi ya klabu yao.

“Tumejipanga kupata matokeo, huwezi kusema tunaenda kushinda au tunaenda kufungwa, huwezi kujua kwa sababu mwisho wa siku ni mipango ya Mungu lakini sisi kama Simba tunakwenda kuhakikisha tunapata matokeo mazuri kwa ajili ya nchi yetu na maslahi ya Simba.”

Simba imeondoka bila nahodha wake John Bocco kutokana na kusumbuliwa na majeraha. Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa siku ya Jumamosi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here