Home Kitaifa Simba ilistahili ushindi kwa Azam

Simba ilistahili ushindi kwa Azam

3885
0

Simba inaendelea kuonesha kwamba inataka kutetea kombe lake la ligi kuu Tanzania bara baada ya kuifunga Azam FC kwa magoli 3-1 na kuendelea kujiongezea pointi kwenye mbio za ubingwa.

Simba ambayo ilikuwa inacheza mchezo wa 18 wa ligi kuu, imefikisha pointi 45 ipo nafasi ya tatu nyuma ya Azam kwa tofauti ya pointi 5 wakati Azam yenyewe imecheza mechi 25. Kinara wa ligi Yanga wenyewe wanapointi 61 tofauti ya pointi 16 na Simba lakini Yanga imecheza mechi 25.

SIMBA INAKIKOSI BORA KWA SASA

Ubora wa kikosi cha Simba kwa sasa hakuna mjadala, Simba wanakikosi bora na wapo kwenye mstari.

MICHUANO YA KIMATAIFA INAISAIDIA SIMBA

Kushiriki mashindano ya kimataifa kumewafanya wachezaji waongeze viwango vyao kutokana na aina ya timu ambazo wanajiandaa kwenda kucheza nazo.

Unajiandaa kucheza na Al Ahly kwenye mechi ya ligi unakutana na Yanga, unajiandaa kucheza na AS Vita ukirudi nyumbani unacheza na Mwadui, unajiandaa kucheza na Saoura unakutana na Azam.

Kwa hiyo utaona namna gani Simba kuwa kwenye michuano ya Champions League na changamoto inazokutana nazo huko zinavyoisaidia timu moja kwa moja inaposhindana na timu za ndani.

WACHEZAJI VIWANGO JUU

Ukiangalia mchezaji mmoja mmoja kuna wachezaji ambao wameonekana kuwa na mwendelezo mzuri wa viwango kitu ambacho ni changamoto kwa wachezaji wengi wa ligi ya Tanzania ambao viwango vyao vimekuwa vya kupanda na kushuka.

Nimeona wachezaji zaidi ya sita (6) ambao viwango vyao vipo kwenye mstari (Meddie Kagere, John Bocco, Pascal Wawa, James Kotei, Aishi Manula, Jonas Mkude, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’) hii inatengeneza balance ya timu upande wa kiwango.

Kuongezeka kwa kiwango na kujiamini kwa beki wa kulia Zana Coulibaly ni faida pia kwa kikosi cha Simba.

SIMBA ILISTAHILI USHINDI VS AZAM

Aina ya magoli ambayo Simba wamefunga ni mazuri, Kagere anafunga goli la kwanza Bocco anafunga la pili kwa kichwa akiunganisha krosi ya Zana Coulibaly Kagere anafunga tena goli la tatu baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Mzamiru Yassin ambaye aliingia tokea benchi na kwenda ku-push mashambulizi.

Dakika 90 Simba inatoka na ushindi wa magoli 3-1 ushindi ambao walistahili kwa namna walivyocheza.

Kwa upande wa Azam naona kwenye mechi nyingi wanacheza wakiwa hawana motivation, wanacheza kukamilisha ratiba. Hata ukiangalia body language za wachezaji hawana ule mwamko tuliozoea kuuona siku za nyuma wanacheza kawaida hakuna kujitoa.

Lakini pia baadhi ya wachezaji naona kama bado wameshindwa kuonesha ubora uliotarajiwa. Kwa mfano Kutinyu sio yule wa Singida United, Enock Atta naye yupo chini, Aggrey na Yakubu walijitahidi kupambana lakini pia Sure Boy kwenye eneo la kiungo alionesha kupambana pamoja na Chirwa eneo la mbele lakini wengine kama hawakuwepo mchezoni.

Sasa tatizo la Azam sijui lipo wapi, ni kocha pamoja na benchi lake la ufundi au uongozi hakuna anayefahamu lakini kwa kifupi sio Azam ambayo tumeizoea.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here