Home Kimataifa “Simba ilicheza Champions League kama mechi ya kirafiki”-Zahera Mwinyi

“Simba ilicheza Champions League kama mechi ya kirafiki”-Zahera Mwinyi

3912
0

Kocha wa Yanga Zahera Mwinyi amesema kwa jinsi alivyoiangalia mechi ya ligi ya mabingwa Afrika AS Vita vs Simba, kiufundi aliona wachezaji wa Simba walikuwa wanacheza kama wapo kwenye mechi ya kirafiki.

Amesema Simba ni timu kubwa lakini namna walivyocheza dhidi ya AS Vita haikuwa kwa ukubwa wa Simba, wachezaji wanapofungwa au kukoswa goli hawazungumzi wao kwao kila mmoja alicheza anavyojua yeye.

“Simba walipoteza nafasi zote mbele, nyuma na katikati, niliona Simba inacheza mechi ya Champions league kama mechi ya kirafiri”-Zahera Mwinyi.

“Watchezaji hawakuwa wanawaza uwanjani kwa namna moja, wote hawakuwa organised kuwaza kwa namna moja kama wakiwa na mpira na wanapokuwa hawana mpira, lilikuwa ni kosa kubwa kwa timu kama Simba.”

“Simba ilipokuwa na mpira iliwategemea wachezaji wa pembeni wangine wote walikuwa wanasimama au wanachelewa kufika kwenye maeneo wanayotakiwa kuwepo wakati timu inashambulia.”

“Ukiangalia kila AS Vita walipokuwa wamepoteza nafasi ya kufunga goli au wamefanikiwa kufunga goli, angalia reaction ya wachezaji wa Simba ilikuwa wapo kawaida hawakasiriki wala kuzungumza wao kwa wao. Wote wanabaki wameshika viuno, hiyo inaonesha kitu gani wanafikiria vichwani mwao.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here