Home Kitaifa Simba, Al Ahly, zaigawa Sports Xtra

Simba, Al Ahly, zaigawa Sports Xtra

5089
0

Kipindi cha Sports Xtra cha Clouds FM kiligawanyika jana usiku wakati wachambuzi wakijadili ni mbinu gani hasa ambayo kocha wa Simba anapaswa kuingia nayo kwenye mchezo wa leo wa CAF Champions League hatua ya makundi dhidi ya Al Ahly ya Misri.

Edgar Kibwana, Geoff Lea, Alex Luambano na Shaffih Dauda kila mmoja alikuwa anavutia kwake mithili ya muwamba ngoma kulingana na ukubwa wa mashindano na aina ya timu ambayo Simba inakutana nayo.

Edgar Kibwana

Uwezo wa Simba kushinda upo, inategemea mwalimu ataingia na approach gani. Ataangalia mapungufu yapi yaliyojitokeza katika mechi mbili zilizopita ambazo timu iliruhusu magoli mengi sana, mechi mbili magoli 10 hii inaonesha namna gani kuna mapungufu makubwa kwenye eneo la ulinzi.

Namna gani atawaheshimu Al Hly na kupanga eneo lake la ulinzi. Mimi ningekua kwenye nafasi yake ningechezesha walinzi watatu kuhakikisha kwamba kuna ulinzi unaofanya wachezaji wa Ahly kupata wakati mgumu kupita ngome ya Simba.

Pia inategemea form ya mchezaji mmoja mmoja ipo katika level ipi, nilikuwepo Misri niliona kocha alitumia mfumo ambao ulimfanya Okwi asionekane. Alikuwa anacheza mbali na goli na wakati huohuo akiwa na jukumu la kumsaidia Kwasi ambaye alipotea katika mechi hiyo.

Kagere alikuwa anazurura muda mwingi kwenye aneo la ushambuliaji la Ahly kwa hiyo kama ataweza kumsogeza Okwi kama alivyofanya kwenye mchezo dhidi ya Saoura Okwi na Kagere wawe karibu na goli la Ahly halafu eneo la katikati kuwe na man to man marking kuwasumbua viungo wa Ahly inawezekana akapata pointi.

Geoff Lea

Mimi natofautiana na Edgar kuhusu sehemu anayopaswa kucheza Okwi, mimi namuelewa kocha kumchezesha Okwi mbali na goli la mpinzani kwa sababu ukiangalia historia nyuma Okwi ni mzuri sana kwa mechi za ugenini ambazo unakuta timu haimiliki mpira lakini unakuta anafunga goli bila kutarajia mfono mechi dhidi ya Setif.

Inawezekana plan ya mwalimu ilikuwa ni hiyo lakini utekelezaji ndio ukamwangusha.

Tukizungumzia mchezo wa Simba vs Ahly moja ya vitu ambavyo sivipendi kuhusu timu za Tanzania zinapocheza dhidi ya timu za ukanda wa Kaskazini tayari imejengeka hizi ni mechi ngumu haijalishi iwe ni timu ya taifa au vilabu hiyo ni kutokana na togauti iliyopo na mfululizo wa matokeo ambao hauibebi Tanzania.

Kitu ambacho Simba wanaweza kufanya, wanaweza kuwa na plan ya muda mrefu na muda mfupi. Hadi sasa hivi Simba ipo chini sana ukiilinganisha na Al Ahly kwa hiyo Simba inatazamwa itapoteza mchezo lakini inapoteza kwa style gani isipoteze kwa matokeo ya kukatisha tamaa.

Kocha hata kama anajua atapoteza lakini swali ni anapotezaje? Hicho ndio anatakiwa kukifanya hata ikitokea anafungwa basi iwe 2-1, 4-2 na ukajifunza kitu.

Namshauri kocha atafute mbinu mbadala ikiwezekana apaki basi, mimi sioni tatizo.

Alex Luambano

Kwa hatua iliyofika Simba, hakuna cha kupoteza kwa sababu imeshafikia malengo yake kwa hiyo wanatakiwa kucheza kadiri wanavyoona wanahitaji kucheza lakini wachukue tahadhari. Basi wangepaki kule (Alexandria, Misri) sio hapa.

Shaffih Dauda

Kwa mtazamo wangu, mwalimu anatakiwa kuwaheshimu Ahly na kutowachukulia poa kama ambavyo mashabiki wengi wanazungumza kwamba Simba wajiachi. Endapo Simba wakifunguka watawarahisishia kazi Ahly lakini kama ikicheza kwa tahadhari itakuwa kwenye mazingira ambayo yatawapa ugumu Ahly kutimiza lengo lao.

Lengo la Ahly ni kuua game dhidi ya Simba na kufuzu hatua ya robo fainali wakijua fika kati ya mechi 3 zilizosalia angalau mchezo dhidi ya Simba wanaweza kutumia nguvu kupata pointi 3 halafu wanasikilizia mechi mbili zitakazobaki.

Wanajua mechi dhidi ya AS Vita pale Kinshasa ni ngumu sana, Vita ni wagumu wanapokuwa kwao hawafungiki kirahisi na mechi ya mwisho na Saoura ni ngumu sana kutokana na historia ya mataifa haya mawili Misri na Algeria.

Upinzani wa Algeria na Misri kwenye soka ni mkubwa sana haijalishi ni timu ya yaifa au vilabu mechi huwa zinakuwa ngumu na hazitabiriki, kwa hiyo kutokana na mazingira ya mechi mbili za mwisho za Ahly lazima watakuwa wamejipanga kulazimisha kupata matokeo dhidi ya Simba.

Uwezekano wa Simba kushinda upo, kwa sababu huu ni mpira wa miguu lolote linaweza kutokea na tumeshuhudia timu kutoka Misri zimewahi kufungwa Tanzania lakini ili matokeo yapatikane inategemea timu ipo kwenye kiwango gani.

Ili timu iweze kushinda dhidi ya Al Ahly lazima iwe kwenye kiwango cha juu, maswali ya kujiuliza kiwango cha Simba sasa hivi kipo juu kiasi kwamba tunaweza kufikiria wanaweza kupambana na Ahly? Kwa hiyo mjadaja ndio upo hapo.

Ni mechi ngumu sana kwa Simba kwa sababu Ahly wanaitolea macho mechi hiyo wanaamini wakikipata matikeo wanatengeneza mazingira ya kufuzu robo fainali.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here