Home Kitaifa Simba 2003 vs 2019 kikosi kipi ni bora?

Simba 2003 vs 2019 kikosi kipi ni bora?

4077
0

Mwaka 2003, Simba SC iliingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kama ambavyo imefanya mwaka huu. Lakini swali ni je, kwa kulinganisha matokeo, kikosi kipi ni bora?

KIKOSI CHA 2003

Juma Kaseja, Athuman Machupa, Boniface Pawasa, Ulimboka Mwakwinge, Selemani Matola, Christopher Alex, Victor Costa, Ramadhani Wasso, Yusuph Macho, Said Sued. Wengine ni Yusuph Macho, Primus Kasonso, Edibily Lunyamila, Lubigisa Lubigisa, nk.

Hadi mchezo mmoja kabla ya kumaliza hatua ya makundi, kikosi hiki kilikuwa kimeshinda 2 (1-0 vs Asec na 2-1 vs Enyimba) na sare moja (0-0 vs Ismailia) katika ardhi ya nyumbani.

Kilipoenda ugenini, kilipoteza mechi zote (3-0 vs Enyimba, 2-1 vs Ismailia). Kilikuwa tayari kimevuna alama 7 na endapo kingeshinda mchezo wa mwisho, kingepata alama 10. Hata hivyo, alama hizi zisingeivusha Simba moja kwa moja kwani ilihitajika muujiza wa Ismailia kushinda ugenini dhidi ya Enyimba ndiyo Simba ipate nafasi.

Simba ikafungwa 4-3 na Asec na kumaliza kundi na alama zile zile 7.

KIKOSI CHA 2019

Aishi Manula, Nicholas Gyan, Mohamed Hussein, Juuko Murshid, Pascal Wawa, James Kotei, Jonas Mkude, Emmanuel Okwi, Clatous Chama, Meddie Kagere, John Bocco. Wengine ni Hassan Dilunga, Zana Koulibally, Asante Kwasi, nk.
Hadi sasa kimeshacheza mechi 5 na kuvuna 6 (3-0 vs JS Saoura na 1-0 vs Al Ahly). Na kimepoteza mechi zote za ugenini (5-0 vs AS Vita, 5-0 vs Al Ahly na 2-0 vs JS Saoura). Kimeshavuna alama 6 na kama kitashinda mchezo wa mwisho dhidi ya AS Vita nyumbani, kitafikisha alama 9 zitakazokifuvusha moja kwa moja.

Kwa matokeo haya, kipi ni zaidi ya kingine?

© Zaka Zakazi

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here