Home Kitaifa Shaffih Dauda ampigia debe Coulibaly Simba

Shaffih Dauda ampigia debe Coulibaly Simba

6867
0

Baada ya ujio wa wachezaji watatu kufanya majaribo kwenye klabu ya Simba, kumekuwa na tetesi huenda beki Zana Coulibaly akaoneshwa mlango wa kutokea endapo wachezaji hao watasajiliwa.

Wachezaji wawili walitamgulia na mwingine akafuata baadaye, kati yao mmoja ni beki na mwingine ni mshambuliaji. Shaffih Dauda anaamini Coulibaly ni mhezaji mzuri lakini alichokosa ni match fitness.

“Kwa nilivyomuona Zana Coulibaly kwenye mechi za Mapinduzi Cup, ni mchezaji mzuri lakini inaonekana hakupata fursa ya kucheza kwa muda mrefu amekosa ‘match fitness”-Shaffih Dauda.

Huo ni mtazamo wangu mimi, inawezakana mtu mwingine ameona tofauti na mimi.

“Nakumbuka Chirwa wakati anaingia Yanga alizingua mechi kadhaa za kwanza watu wakamkataa lakini baadaye aka-click kilichofuata ni historia.”

“Alikuja pia Justice Zulu ‘MkataUmeme’ akawasha moto mwingi kwenye mechi yake ya kwanza baada ya pale hakuwa na mwendelezo mzuri kwenye mechi zilizofuata lakini inaelezwa kabla ya kujiunga na Yanga hakuwa amecheza mechi za mashindano kwa miezi 6 inawezekana Yanga walishindwa kumpa muda.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here