Home Dauda TV Shaffih Dauda aeleza kilichoiua Simba Congo

Shaffih Dauda aeleza kilichoiua Simba Congo

8487
0

AS Vita walianza taratibu wakiwa wanaisoma Simba, walitengeneza nafasi na kufanya mashambulizi kadhaa ya kushtukiza huku wakitumia udhaifu wa safu ya ulinzi ya Simba.

Eneo la katikati ya uwanja AS Vita walionekana kuwa na nguvu sana na walifanikiwa kuliteka eneo hilo na kuwa sehemu yao ya kuanzishia mashambulizi.

Kadiri muda ulivyokuwa unasonga walikuwa wanaongeza kasi ya mchezo na kushambulia kupitia pembeni hali iliyowafanya mabeki wa Simba kuvurugika na kusababisha Vita kutengeneza nafasi nyingi za kufunga.

Baada ya kugundua timu wanayocheza nayo inaweza kuwapa nafasi nyingi za kufunga wakawa wanaendelea kutengeneza nafasi za kufunga na kama wangetumia vizuri nafasi walizotengeneza huenda wangefunga zaidi ya mabao matano.

Maoni yangu baada ya mchezo wa AS Vita vs Simba nimeyaweka #YouTube kwa kirefu zaidi tembelea #DaudaTV

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here