Home Kimataifa Serie A is Back (Baba mtakatifu angesemaje dili la Ronaldo?)

Serie A is Back (Baba mtakatifu angesemaje dili la Ronaldo?)

8119
0

Hapo zamani za kale Italia ilikuwa na watu wabaya kwenye soka la ulaya. Walijua kushawishi sana wachezaji. Alikuwepo mwanaume aliyejulikana kama Silvio Beluscone na kule Turin alikuwepo mbabe wa kupanga matokeo Lucciano Moggi. Miaka ile Juventus na Ac Milan ulikuwa huwezi kabisa kubishana nao kwenye suala la manunuzi. Moggi ndiye aliyemleta Zlatan Juventus kibabe.

Beluscone amewahi kushtakiwa kwa makosa sio chini ya 20 likiwepo la €560m dhidi ya kampuni zake. Alipoondoka tu wachezaji muhimu kama Andrea Pirlo, Zlatan Ibrahimović na Thiago Silva waliondoka na nafasi zao kuchukuliwa na wachezaji waliokuwa hawana hadhi ya kuchezea Milan kama Alessandro Matri, Philippe Mexès na Cristian Zapata. Hadhi ya Milan ilishuka hadi kufikia zama za 1986.

Serie A ilitisha kwa majina makubwa kama Diego Maradona alipoungana na Michel Platiniin miaka 1980s. Wakali kama Paul Gascoigne, Lothar Matthaus, Dennis Bergkamp, Ronaldo Nazario na Zinedine Zidane

Tokea mwaka 1982, ligi kuu italia ilikuwa ikivunja rekoddi ya manunuzi lakini sina uhakika kama zama hizi itaweza kuvunja rekoddi ya Neymar ys €222m,

Ni miaka 17 tokea Serie A iweke rekodi hata hivyo mwaka 1984 na 2000 Italia walivunja rekodi ya manunuzi na mauzo mara 9 mfululizo.

1984: Diego Maradona – Napoli kwenda Barcelona [€6.9m, ikapanda mpaka €16.2m kutokana na uporomokaji wa thamani ya Euro]

Diego Armando Maradona alivunja rekod mara mbili, wakati anatoka Boca Juniors kwenda Barcelona na aliporudi Napoli.

El Pibe d’Oro aliwasaidia Partenopei’s kushinda Scudetti na UEFA Cup.

Neymar ana thamani ya Maradona 13 Maradonas:

1987: Ruud Gullit – PSV kwenda Milan [€7.3m, €17m]. Gullit alisajiliwa mara tu Silvio Berlusconi alipoichukua Milan.

1990: Roberto Baggio – Fiorentina kwenda Juventus [€8.3m, €18.3m]

Baggio alipoondoka Florence mitaani vurugu nyingi sana zilizuka sana licha ya Viola kupokea mamilioni ya fedha.

Mr Il Divin Codino alifanikiwa kufunga mabao 115 kwenye michezo 200 na kuisaiidia Juve, kushinda UEFA Cup 1993 na Serie A mwaka 1995.

1992: Jean-Pierre Papin – Marseille kwenda Milan [€12.5m, €20.8m]

Milan walivunja rekodi ya Juventus jwa kumsajili msshambuliaji huyu wa Marseille’s Jean-Pierre Papin, lakini alicheza misimu miwili tu na Rossoneri. Alifunga mabao 31 kwenye michezo 63 lakini alisumbuliwa sana na majeraha kabla ya kutimkia Bayern Munich mwaka 1994.

1992: Gianluca Vialla – Sampdoria kwenda Juventus [€13.4m, €25m ].
Pale Turin Vialli alifanikiwa kushinda kila kitu pamoja na Champions League mwaka 1996. Na ndiye nahodha wa mwisho Bianconeri kushinda taji hilo.

1992: Gianluigi Lentini – Torino kwenda Milan [€14.1m, €27m]. Pope John Paul II alikerwa sana na ada ya uhamisho ya Lentini kwenda Milan kama “an offence to the dignity of work” (Matusi kwenye utu wa kazi” alipokuwa akiongea kule Ex Cathedra wakati huo.

1997: Ronaldo – Barcelona kwenda Inter [€24.7m, €35.7m]. Ronaldo alifanikiwa kufunga mabao 47 kwenye michezo 49 akiwa Barcelona. Inter walipatwa na mikosi katika misimu miwili De lima alishindwa kushiriki vyema baada ya kuumia goti. Akabeba Scudetto mwaka 2002, kisha kuwa mfungaji bora wa kombe la dunia na kutimkia Real Madrid.

1999: Christian Vieri – Lazio kwenda Inter [€49m, €56m ]
2000: Hernan Crespo – Parma kwenda Lazio [€55m, €60.2m]

Msimu wa 2009 Rossoneri’ walimpoteza Beluscon, Ancelotti akatimkia Chelsea, kipenzi chao Kaká akakwea pipa kwenda Real Madrid. Wakaanza kuja makocha waliofeli, Leonardo, Max Allegri, Clarence Seedorf, Pippo Inzaghi, Siniša Mihajlović, Cristian Brocchi, Vincenzo Montella na sasa Gennaro Gattuso ambao wengi wao sio makocha wakubwa.

SERIE A MPYAAA INAKUJA

Baba mtakatifu John Paul alikuwa shabiki mkubwa wa soka licha yakwamba alikuwa akishabiki vilabu vingi.

Mashabiki wa Fulham wanadai alikuwa shabiki wao, lakini Kipa wazamani wa Liverpool nae anasema Baba mtakatifu huyo akikuwa shabiki wao na aliwahi kumwambia. Lakini upande wa Barcelona wanadai kuwa Papa huyo alipewa kadi ya uanachama ya klabu hiyo namba No 108,000 aliyopewa pale Nou Camp stadium, in mbele ya mashabiki 120,000 Novemba 1982.

lakini hili halikumzuia kuongelea usajili wa Lentini.

Baba mtakatifu John Paul II aliyekasirishwa na usajili wa Lentje angekuwepo usajili wa Ronaldo wa Euro Miloni 299 angesemaje achilia mbali dili ya Higuain la Euro 75 m kwenda Juventus. Au Vatcan ingekuwa Paris apate taarifa kuna kijana wa Brazil wa miaka 25 amesajiliwa Euro 200m??

CR7 ameenda Juve na kujaribu kurudisha ile hadhi ya 1990, ambapo vilabu vya Italia vilisshiriki takriban fainali 25 katika michuano mbalimbali ya UEFA na kutwaa vikombe 13.

Skendo za Calciopoli zilipunguza hadhi ya ligi hiyo na kushindwa kuvutia wawekezaji.

Takwimu za matumizi ya fedha mpaka sasa katika ligi 5 bora

Premier League: 1.042 billion 💶
Serie A: 895 millon 💶
LaLiga: 453m 💶
Bundesliga: 414m 💶
Ligue 1: 375m 💶

Cristiano Ronaldo amepandisha dau lao mpaka kufika 895 million 💶, na kuzipiku ligi za Spain, France na Germany.

Napoli inajipanga vyema

Napoli imepoteza kocha wao mkuu Maurizio Sarri na nyota Jorginho kwa klabu ya Chelsea. Ujio wa Carlo Ancelotti huenda ukawarudisha tena kwenye raman Partenopei.

Roman ndani ya himaya mpya

Monchi ndiye mkurugenzi wa klabu hii. Roma wamewekeza 110m 💶. Wameshapokea fedha kutoka kwa kipa wao Alisson Becker aliyetimkia Liverpool. Pia wamemnasa kinda Justin Kluivert na mkongwe Javier Pastore.
Hivi majuzi walikuwa mbioni kunasa kandarasi ya Malcom kabla ya kupokonywa na Barcelona

Matumaini ya Inter

Waliwabwaga Roma kwa kumpata kiungo wao bora Radja Nainggolan. Pili wamefanikiwa kurudi Champions League. Lautaro Martinez na Stefan de Vrij tayati wameshajiunga na klabu hiyo huku wakimfukuzia Arturo Vidal pamoja na mchezaji bora wa kombe la dunia Luke Modric. Nerazzurri are back

Mabwenyenye wa Milan

Matajiri wa AC Milan walifanikiwa kukwepa rungu la Financial Fair Play ili kuokoa nafasi yao ya kushiriki Europa League. Gonzalo Higuain yupo mbioni kutua klabuni hapo.

San Siro kimenuka waambieni ligi ya Italia imerudi..

Hapa upo kwenye website ya Shaffih Dauda, pia tuna ukurasa wa Instagram na facebook kwa jina hilo hilo, huko utakutana na taarifa nyingi na za uhakika. Usiache kutembelea YouTube channel yetu ya Dauda Tv.

Mimi naitwa Privaldinho (Instagram)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here