Home Kitaifa Serengeti Boys yawapa kombe watanzania

Serengeti Boys yawapa kombe watanzania

4120
0

Timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 imeshinda kombe la Ukanda wa COSAFA baada ya kuwafunga Angola katika mchezo wa fainali uliomalizika kwa sare ya kufungana 1-1 na kuamuliwa kwa matuta ambapo Serengeti Boys ikaibuka mshindi kwa penati 6-5.

Kocha mkuu wa timu hiyo Oscar Milambo amesema vijana wanahitaji pongezi kwa kazi waliyoifanya na kulipa heshima taifa.

“Vijana wamefurahi baada ya kufanya kazi nzuri na tunawapongeza kwa hicho walichokifanya lakini pia benchi la ufundi kwa umoja wao na ushirikiano na maelekezo ambayo wamekuwa wanayatoa kwa vijana mwisho wa siku wametuletea heshima kubwa Tanzania”-Oscar Milambo, kocha Serengeti Boys.

“Tunaamini haya matokeo ni nguvu zao lakini pia kitu kikubwa ambacho kipo ni support ya watanzania waote ambao mwisho wa siku tunawapelekea kikombe na tunaamini itakuwa furaha kwa wote.”

Katika hatua ya makundi timu hizo zilipokutana  Angala iliifunga Serengeti Boys 2-0.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here