Home Kimataifa “Senegal bila mimi hafui dafu” Diof

“Senegal bila mimi hafui dafu” Diof

3876
0

SENEGAL

Mshambuliaji wa zamani wa Senegal Al hadj Diof amesema kuwa maoni yake yana msaada mkubwa kwa Senegal ili ishinde AFCON yeye anahitajika sana.

“Maoni yangu yanahitajika kwenye mchakato wa kuisaidia wa Senegal kufanya vizuri”

Diof mwenye umri wa miaka 38 kwa sasa amesema haitaji kuwepo kwenye benchi la ufundi lakini mchango wake unahitajika sana. Diof mara ya mwisho alionekana uwanjani kwenye mechi ya kiushindani msimu wa 2014-15 akiwa na klabu ya SABAH FC ya nchini MALYASIA.

Mara kadhaa amekuwa akishiriki mazoezi na kikosi cha Senegal. Diof na aliou Cisse ni marafiki wakubwa. Hapo awali walifanya makubwa kwenye kikosi chao kwenye kombe la dunia 2002 chini ya kocha Bruno Metsu marehemu.

Hapo awali Cisse na Diouf walikuwa na ugomvi mkubwa sana. Diouf alikiri kuwepo na tofauti hizo

“Mimi na Cisse tulipishana kauli na mtazamo kama watu wemgine. Tulipokutana kila mtu alimweleza mwenzake ukweli na tukamalizana kiume”

“Kwa sasa hatuna shida tupo sawa na nipo tayari kufanya nae kazi”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here