Home Kimataifa Sasa Golden State Warriors Wanaweza Kushusha Pumzi Juu ya Kocha Wao, Steve...

Sasa Golden State Warriors Wanaweza Kushusha Pumzi Juu ya Kocha Wao, Steve Kerr.

1942
0

Kumekuwepo na maswali mengi juu ya namna mabayo wachezaji wa klabu ya Golden State Warriors wanaweza kuendana na mbinu za kocha msaidizi wa klabu hiyo Mike Brown hasa wakati ambao wanakuwa na presha ya kutokocheza vyema.

Hii ilitokana na kutokuwepo kwa kocha mkuu wa klabu hiyo Steve Kerr ambaye alipata maumivu ya mgongo, likiwa ni tatizo ambalo lilimsumbua pia mwishoni mwa msimu uliopita. Tatizo hili lilimweka nje mwanzo mwa msimu uliopita na lilipojirudia msimu huu lilimfanya akose mwanzo mwa hatua za mtoano dhidi ya klabu ya Portland Trail Blazers.

Hata hivyo taarifa za kitabibu zinaonyesha kuwa kocha huyo yupo mbioni kurejea kwenye hali yake ya kawaida na kuisimamia timu hiyo baada ya taarifa kutoka leo Jumatano kuwa atasafiri na klabu yake kuelekea kwenye mchezo wa tatu dhidi ya San Antonio Spurs ikiwa ni mwendelezo wa fainali ya kanda ya Magharibi wakiwa wanaongoza kwa ushindi wa michezo miwili ya mwanzo tayari.

Warriors wamesema wanaendelea kumpa muda kocha huyo mkuu mpaka pale atakaposema kuwa yupo sawa kuendelea kuifundisha timu hiyo na kuendelea na shughuli zote za kila siku hivyo hawajaweka wakati sahihi wa kurejea kwake. Lakini kumekuwa na maendeleo mazuri kwani hayupo mbali tena na timu bali huzungumza na kocha mkuu wa muda ambaye pia ni msaidizi wake Mike Brown kwa njia ya simu.

Na katika michezo miwili ya kwanza ya fainali alitizama mchezo akiwa kwenye vyumba vya kubadili nguo huku pia akiwepo kwenye mazoezi. Mkurugenzi wa klabu hiyo Bob Myers amethibitisha kuwa Kerr atasafiri Jumatano wakati akiwa anafanya mahojiano na redio ya  Bay Area kwenye kipindi cha The Game.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here