Home Kimataifa Sarri “Papai linakaribia kuiva muda wowote linadondoka”

Sarri “Papai linakaribia kuiva muda wowote linadondoka”

3837
0

Kwa sasa anaonekana ni kama mtu anaetembea akiwa amekufa, je?, anae wa kumlaumu au ndo aliyataka mwenyewe!. Anajikokota kutoka katika msukumo wa mashabiki pamoja na waandishi wa habari. Lakini timu yake inaonyesha kucheza vizuri, je! Nini kinaenda kombo?. Anajiuliza , tumefikaje hapa!, wakati nimekua na mwanzo wa msimu mzuri. Na ikumbukwe tuuh, Anaushindi mkubwa kuliko Pep Gurdiola katika msimu wake wa mwanzo. Na ndie anaeongoza katika historia ya klabu kwa kuwa na mwanzo mzuri wakuto fungwa katika michezo 11 ya mwanzo.Kocha mkuu wa Chelsea fc, Maurizio Sarri anayoyapitia kwa sasa yanafanana na tuliyo yaona kwa Luiz Felipe Scolari au Andre Villa Boas kwa miaka ya nyuma?. Sarri anatiwa msumari wa kichwa na maneno ya bosi wa Chelsea fc alipohojiwa na wanahabari alisema “sijui maana ya Sarriball, kama nIlivo sema hapa Uingereza ni mara ya kwanza, sijui sarriball ni nini.” Anaendelea… “nafikiri imetoka kwenye masijara ya Italia, sijawai kusikia hicho kitu” akaongezea “sijajua (kama itakua rahisi nje ya klabu) nafikiri, ifike tamati kitu muhimu ni matokeo, katika kazi yangu nahitaji matokeo. Na si kitu kingine”Pep Gurdiola kashangazwa na utamaduni ya klabu ya Chelsea, nae amenukuliwa akisema “hali (ya Sarri) ilikua na tofauti kidogo na yangu, mwaka wangu wa kwanza, klabu (Man city) haikunitilia shaka, haikua katika vyombo vya habari kwamba nitafukuzwa kazi endapo nitapoteza mchezo huu au mchezo mwingine, haikutokea. Nilishangazwa Conte kushinda ligi (misimu 2 iliyopita) na walipoteza michezo mmoja au miwili mwanzoni mwa msimu uliofuata, watu wakaanza kusema atafukuzwa!” alipo ulizwa kuhusu kipigo alichompa Sarri cha 6-0 akajibu “tulipo poteza 2-0 nyumbani kwao huwezi kubali kushindwa nyumbani. Itabaki kuwa hivo, tutaenda kucheza fainali (Carabao cup) tukijaribu kuboresha mtindo wa kucheza ili tuweze kushinda”. Hii ni jaribio la kwa Sarri endapo atapigwa na City, na siku tatu baadae na Tottenham katika mchezo wa ligi basi ataambiwa abebe vilago vyake.Yeye kwa upande wake amegundua wachezaji wake hawana imani, hii ni katika mchezo wa Europa waliocheza dh`idi ya Malmo na kuibuka na ushindi wa 3-0. Na aliwataka wajisikie huru katika akili zao. Amenukuliwa “katika hii mechi, dakika 30 za mwanzo nimeona timu ilikua na uwoga. Kwa hiyo sitaki kuwasukuma kucheza, nataka akili zao ziwe huru. Tutajianda na hilo katika mechi ya jumamosi”… aliongeza “sikupenda akili mtazamo wetu katika dakika 30 za mwanzo, nahitaji kitu huru. Hivyo tutajiandaa na dakika 60 na zaidi”Klabu ya Chelsea inamtolea jicho la tatu alikua kocha msaidizi wa timu ya taifa la Uingereza, Steve Holland kama mtarajiwa mbadala wa Maurizi Sarri endapo atashindwa kukiokoa kibarua chake. Holland ameonekana kama ni chaguo la kwa kwanza kwa Chelsea kwa kushikiria uskani na kuiongoza klabu hiyo kwa msimu ulio bakia 2018-19. Japo ushindi katika mechi ya Europa league imepunguza mgandamizo na kumfanyia wepesi kwa nafasi aliyopo kwa sasa. Kapewa mechi mbili tuu, akishindwa zote. Itakua ndo mwisho wa habari.Wahenga wanasema, majuto ni mjukuu na huja baadae. Ninachokiona mimi hapa Chelsea watakumbuka alichokua anajaribu kukileta Maurizio sarri katika sura ya mpira wa miguu nchini uingereza na klabuni hapo. Anahitaji muda, na si kuafanishwa na kocha Fulani, au upangaji wake wa kikosi na upangaji wa timu nyingine. Kuwa nje ya timu bora 4 za msimamo kwa pointi moja (United) na kuwa sawa na timu ya tano (Arsenal) si jambo baya. Safari bado ni ndefu na timu bado inafanya vizuri. Na ukizingatia Chelsea ipo kikaangoni na hati hati ya kutosajiri kwa misimu miwili mfululizo kufatia udanganyifu katika usajiri wao. Japo wanaweza kuvuta muda kwa rufaa itayowawezesha kusajiri dirisha kubwa. Lakini bado watakua wameshikilia bomu linalo hesabu dakika kulipuka.MWANDISHI : ISACK MSINJILI

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here