Home Kimataifa Sarri anawagawa Chelsea

Sarri anawagawa Chelsea

5939
0

Makala na Raphael Lucas
Kocha mkuu wa Chelsea maurizio Sarri bado amekua kwenye minong’ono mikubwa kwa mashabiki wa the blues, na hii inatokana na matokeo ya kutoridhisha ya hivi karibuni. Wikendi iliyopita Chelsea imetoka kupoteza mchezo wao dhidi ya washika mitutu wa London club ya Arsenal.

Discussion sio kubwa kuhusu matokeo, kinachojadiriwa zaidi ni Pasi zaidi ya 2000 zilizopigwa na kiungo mkabaji Jorginho pasipo kua na asisti, Rio Ferdinand alipoulizwa kuhusu hiki alisema “kiungo mwenye Pasi zaidi ya 2000 bila asisti unasemaje kiungo bora zaidi ya kupiga Pasi za upande na za karibu karibu” haya maneno ndiyo yanayosemwa zaidi na mashabiki wa Chelsea ambao mpaka sasa washajigawa kuna wale wanaosema sarri hana jipya na wanaosema bora wakati wa conte.

Jorginho ndo injini ya Sarriball lakini imekua imezoeleka kwa timu pinzani kwa sasa kuchukua matokeo dhidi ya Chelsea kwani wapinzani wamekua wakiingia kumnyima Jorginho uhuru wa kucheza pamoja na kumficha Hazard ambaye kwa siku za hivi karibuni amekua akitumika Kama namba 9 ambapo sio namba ake kiasili kwani ye hupenda zaidi kutokea pembeni na ili awe na wigo mkubwa wa kuchezea mpira.

Mashabiki wengi wa Chelsea wanaamini Ngolo Kante ni Bora zaidi ya Jorginho hasa kwenye kuiletea timu muunganiko na matokeo kwa ujumla kitu ambacho ni tofauti na msimamo wa Sarri, kumbuka misimu miwili iliyopita wakati Ngolo Kante akizichezea club za Leceister city na Chelsea wakati wa Conte alikua akifanya vizuri zaidi pale anapocheza Kama kiungo mkabaji na sio mchezeshaji Kama anavomtumia Sarri

Usajiri wa Higuain hauwezi kuja kua mwarobaini wa Chelsea kwa sasa mpaka pindi watapojiimalisha upande wa beki line yao na kiungo kwa ujumla, pamoja na Morata na Giroud kulaumiwa sana kwa kukosa nafasi za wazi hasa mzunguko wa kwanza lakini naamini Ngolo Kante anahitajika kurudi kwenye eneo lake asilia.

Raphael Lucas(udom)
0710690782/0764764449

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here