Home Ligi EPL Sakata la Pogba kuondoka United lachukua sura mpya, anarudi Serie A?

Sakata la Pogba kuondoka United lachukua sura mpya, anarudi Serie A?

11722
0

Kumekuwa na sinema ambayo bado hakuna anayejua mwisho wake kati ya kiungo wa Manchester United Paul Pogba na klabu yake hiyo haswa kocha waoa Jose Mourinho.

Ilianza kama fununu ambayo kila siku inaonekana kuzidi kuwa kubwa ikimuhusisha Pogba kuondoka Manchester United kwa kile kinachotajwa kukosa furaha ndani ya klabu hiyo.

Hii leo sasa kumekuja taarifa mpya ambazo zinasema wakala wa mchezaji huyo Mino Raiola amepanga kukutana na Juventus mwezi December ili kulimaliza suala hili.

Raiola anakutana na Juventus ikiwa ni sehemu ya jaribio la kumrudisha Paul Pogba Juventus, klabu ambayo ndipo alitoka kabla ya kujiunga na Manchester United.

Kwanza inadaiwa Juventus wanataka kumuongezea mkataba mshambuliaji wao Moise Kean ambaye pia ni mteja wa Raiola na katika mazungumzo kuhusu Kean wamepanga kujadili namna ya kumpata Pogba.

Alhamisi iliyopita Pogba alinukuliwa akisema yeye ni mchezaji wa Manchester United kwa sasa na kuweka wazi kwamba hajui nini kitatokea kwake siku za mbeleni.

Suala la Raiola kukutana na Juve kwa ajili ya Pogba ni mjadala mkubwa Italia kwa sasa huku jarida la Tutto Sports likithibitisha kuhusu Raiola na Juve katika toleo lao la jana.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here