Home Ligi EPL Sahau kuhusu PSG na Man City, hii ndio timu yenye safu kali...

Sahau kuhusu PSG na Man City, hii ndio timu yenye safu kali ya ushambuliaji ulaya

6969
0

Ilikuwa ikitegemewa kwamba klabu ya Paris Saint Germain ingekuwa moja ya timu ambayo ingekuwa kiwembe kwenye suala la ufungaji msimu huu, lakini hakuna aliyedhani Lyon FC ndio ingekuwa klabu ambayo ingekuwa na safu kali ya ushambuliaji kwenye ligi 5 kubwa barani ulaya.

Nabir Fekir, Mariano na Memphis Depay wamekuwa kwenye kiwango bora msimu huu, wamefunga jumla ya magoli 26 katika Ligue 1, idadi kubwa zaidi ya ile ya washambuliaji wa PSG – Kylian Mbappe, Edinson Cavani na mchezaji ghali zaidi duniani – Neymar ambao kwa ujumla wamefunga magoli 24 katika ligi.

Mariano amewasili kutoka Real Madrid na tayari ameweza kufiti vizuri ndani ya mfumo wa timu, uwezo wake wa kupangua ngome na kutengeneza mianya kwa Fekir kuitumia

Wafungaji bora wa Lyon msimu wa 2017/18

1 Fekir: 11 goals

2 Mariano: 9 goals

3 Depay: 6 goals

Manchester City wamekuwa wakisifiwa kuwa klabu inayocheza soka la kuvutia zaidi kwa sasa chini ya Pep Guardiola na timu yao imefunga zaidi ya magoli 50 kwenye mashindano yote msimu huu.

Hata hivyo Safu ya ushambuliaji ya City inayoundwa Sergio Aguero, Gabriel Jesus na Raheem Sterling wamefunga magoli 22 mpaka sasa katika Premier League pekee.

Ushindi wa Lyon wa 5-0 dhidi ya wapinzani wao Saint Etienne ulikuwa ni mjumuisho wa kiwango kizuri cha Lyon msimu huu.

Wakicheza katika uwanja wa ugenini, safu ya ushambuliaji ya Lyon ilionyesha wazi makali yao – wakifunga magoli 4 kati ya hayo matano.

Fekir alifunga magoli mawili, Mariano aliongeza moja, Memphis akafunga lingine na Oscar Garcia akaweka msumari wa 5.

Hata hivyo Lyon sio timu inayoongoza kwa kufunga magoli mengi nchini Ufaransa katika mashindano yote, wamefunga magoli 32 kwa ujumla – washambuliaji wake wakichangia 81.25% ya magoli hayo.

Utegemezi mkubwa wa wachezaji hawa watatu unaweza kuleta tatizo endapo mmoja wao atapata majeruhi, hata hivyo vijana hawa watatu kwa sasa wanaibeba timu yao mabegani na huenda wakaendelea kuweka rekodi msimu huu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here