Home Ligi EPL Rui Faria ameondoka na furaha ya Mourinho, na leo Madrid wanaweza kuharibu...

Rui Faria ameondoka na furaha ya Mourinho, na leo Madrid wanaweza kuharibu kabisaa

15869
0

Usiku wa kuamkia Jumatano(usiku wa leo) klabu ya Manchester United watakuwa uwanjani kuwakabili Real Madrid katika mchezo katika muendelezo wa michuano ya ICC.

Mchezo huu wengi wanauona kama mchezo wa kirafiki tu lakini ukiungalia nje ya box ni mchezo ambao una maana kubwa sana kwa Manchester United haswa kwa kocha wao Jose Mourinho.

Mourinho hafurahii kufungwa na timu kubwa popote pale na ndio maana kipigo cha mabao 4-1 kutoka kwa Liverpool kilizua habari nyingi sana na yote haya yalitokana na maneno ya Mourinho.

Kama United watafungwa katika mchezo wa leo inamanisha watakuwa wamefungwa mara mbili mfululizo katika mechi zao za maandalizi ya msimu mpya wa EPL jambo ambalo litazua taswira nyingine mpya kuelekea msimu ujao wa EPL.
Paul Pogba, Romelu Lukaku, Marouane Fellaini, Marcus Rashford, Jesse Lingard, Ashley Young, Phil Jones, Victor Lindelof na Marcos Rojo bado hawajarudi, Nemanja Matic na Valencia wameumia, Anthony Martial yuko Ufaransa na presha kwa Mou inazidi kuwa kubwa.

Rui Faria naye bado anamuumiza sana Mou.

Rui Fillipe “Da Cunha” Faria ni raia wa Ureno, huyu amekuwa pembeni ya Mourinho tangu Jose aanze soka la kupambana sana mwaka 2002/2004 akiwa na Fc Porto.

Faria kwanza alikuwa kocha wa viungo wa Porto akaondoka na Mourinho kwenda Chelsea 2004 kama msaidizi, wakaenda Inter tena mwaka 2008, mwaka 2010 wakaenda wote Real Madrid, 2013 wakaenda Chelsea kabla ya 2016 kujiunga na Real Madrid.

Inasemekana Faria ndiye mtu ambaye anamjua Mou kuliko mwanadamu yeyote katika soka, furaha na huzuni za Mou katika soka alikuwepo na ndiye msaada mkubwa hadi Mou anabeba makombe 25.

Nyota wa zamani wa Liverpool Charlie Adam amenukuliwa akisema kuondoka kwa Faria lazima kuiathiri Manchester United na hili pia litaleta mtikisiko mkubwa kwa Mourinho katika msimu unaokuja.

Tangu Faria aachane na Mourinho, kocha huyo wa United anaonekana kukosa furaha na kuwa na mikwaruzano na mabosi kila kukicha, tayari Mou amewaweka katika bodi ya ufundi Michael Carrick na Kieran McKenna kuziba nafasi ya Faria.

Makombe ambayo Mourinho na Faria walishinda.

2002/2004 Fc Porto 6 (Kombe ya ligi 2, kombe la chama cha soka 2,Champions League 1, Europa 1).

2004/2007 Chelsea 6(Kombe la ligi 2, Fa 2).

2008/2010 Inter Milan 5(Kombe la ligi 2, Michuano ya Italia 2, Champions League 1).

2010/2013 Real Madrid 3(Kikombe cha ligi 1, Michuano ya Hispania 2).

2013/2015 Chelsea 2(Kikombe cha ligi 1, Michuano mingine Uingereza 1).

2016/Sasa Manchester United (Michuano mingine Uingereza 2, Europa 1).

Madrid wameshamkata kilimilimi.

Kama unafahamu nikukumbushe ya kwamba United walikuwa kwenye mbio za kumnasa Gareth Bale, kwa mda sasa wamekuwa wakihusishwa kumnunua nyota huyo kutoka Rea Madrid.

Lakini hii leo wakati wakijiandaa na mchezo wao dhidi ya Manchester United, kocha wa Real Madrid Julen Lopetegui amesema Bale ana furaha sana Real Madrid na yuko tayari kuvaa viatu vya Cristiano Ronaldo.

Nani Mbabe kati yao?

Real Madrid ndio wababe wa Manchester United kwani katika mechi 11 ambazo timu hizi mbili zimekutana, Madrid wameshinda mara 5, Manchester United wameshinda michezo miwili huku timu hizi zikienda suluhu mara 4.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here