Home Kitaifa Ruge apumzishwa makazi ya milele

Ruge apumzishwa makazi ya milele

2964
0

Mchanga umemeza mwili wa Boss wetu, lakini hautaweza kumeza roho yake, hautaweza kumeza mawazo na fikra chanya alizoambukiza kwa Taifa lake.

Hapa ndipo ulipolala mwili wa #JasiriMuongozaNjia: roho yake iko pamoja nasi.

Na maua haya ni ishara ya upendo, heshima, dua na shukrani kwa #JasiriMuongozaNjia.
.
Waombolezaji mbambali wakiweka maua katika kaburi la mpendwa wetu #RugeMutahaba.

Watoto wa mpendwa wetu Ruge Mutahaba wakiweka maua kwenye kaburi la baba yao huku huzuni ikiwa imetanda mioyoni mwao.

Mama nyamaza usilie kwani mtoto wako Ruge Mutahaba alisema akitangulia mbele za haki tusilie bali tusherehekee najua ni ngumu lakini hatuna budi kushukuru Mungu kwa kila jambo.

Mioyo imeingia mchanga, Maumivu yameshamiri, Machozi hayazuiliki. #JasiriMuongozaNjia Kaenda.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here