Home Kitaifa Ruge alivyopokelewa na kuagwa Bukoba

Ruge alivyopokelewa na kuagwa Bukoba

2723
0

Hivi ndivyo wakazi wa Bukoba walivyojitokeza ‘BukobaAirpot’ huku nyuso zao zikiwa na simanzi ili kuweza kuupokea mwili wa mpendwa wao/wetu Ruge Mutahaba.

Magari yamepambwa, ikiwa ni ishara ya kuonyesha upendo wao kwa mpendwa wetu Ruge Mutahaba, Bukoba imezizima, huzuni imetawala.

Brigedia Jenerali Marco Gaguti Mkuu wa Mkoa wa Kagera amefika uwanja wa ndege kuongoza mapokezi ya mpendwa wetu Ruge Mutahaba. Kabla Brigedia Jenerali Marco Gaguti kufika hapa Kagera alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe kipindi kile alikuwa ni Kanali kabla ya kupanda cheo amefanya kazi za kizalendo bega kwa bega na Ruge Mutahaba mojawapo ikiwa ni Fursa na Ile ya Umoja wa Mataifa Kigoma Programu ya pamoja.

Watoto ambao walitamani kukuwa na kuishi wakimsikiliza na kutengeneza hoja na mpendwa wetu Ruge Mutahaba nao wamejitokeza na wazazi wao ili kuupokea mwili wa mpendwa wetu Ruge Mutahaba.

Picha mbalimbali zikionyesha mwili wa mpendwa wetu, Ruge Mutahaba ukiwasili katika uwanja wa ndege wa Bukoba “Bukoba Airport’ tayari kuelekea nyumbani ambapo kesho utapumzishwa kwenye nyumba yake ya milele.

“Hata sisi tunataka kumuaga mpendwa wetu Ruge Mutahaba” Ni kama vile wanasema hawa #WanaKagera ambao wamepanda juu ya mti kushuhudia mpendwa wetu akiagwa, mazishi yatakayofanyika kesho Jumatatu.

Wakazi wa mji wa Bukoba hawaamini kabisa kama mtoto wao Ruge Mutahaba tamati ya maisha yake imefika. Wamejitokeza kwa wingi kuulaki mwili wa kijana wao.

Mwili wa mpendwa wetu Ruge Mutahaba tayari umefika uwanjani #Gymkhana hapa Bukoba kwa ajili ya sala na salamu za mwisho.

Ulitufundisha Upendo ni ngumu kuamini uliyoyatenda yatabaki kwenye kumbukumbu vizazi hadi vizazi…! Pichani Mkurugenzi wa Biashara na Uwekezaji Shebba Kussaga akifuta msalaba wa rafiki na Mkurugenzi mwenza katika Vipindi na Uzalishaji Ruge Mutahaba.

Mshumaa uliwaka na kuleta mwanga, Mshumaa ulileta nuru, Mshumaa ulileta tabasamu , Mshumaa ulileta uhakika na ulileta faraja lakini gafla umezima na kuleta simanzi, huzuni na taifa kuzizima kwa vilio vya kila sehemu kwa maumivu baada ya mshumaa kuzima.

Familia ya Ruge Mutahaba, ikiwa tayari ipo hapa uwanja wa #Gymkhana Bukoba, kwa ajili ya kufanya sala na kutoa salamu za mwisho kisha kumpumzisha mpendwa wao/wetu Ruge Mutahaba.

Licha ya huzuni kuwatawala lakini walihakikisha wanafanya kile ambacho Baba yao anakipenda kuwaona wanafanya kwa wakati wote. Watoto wa Ruge Mutahaba (Wasanii wa THT) Wakimuimbia Baba yao ambaye amelala usingizi mzito mbele yao.

“Kama kila mmoja aliyeguswa hapa ataamua kusaidia angalau Watanzania wawili/watatu pengo lake linaweza kuzibwa” Mwachi Mutahaba.

Wasanii mbalimbali waliosafiri kutoka DSM na maeneo mengine kuja Bukoba kumsindikiza #RugeMutahaba katika safari yake ya mwisho.

“Ruge hakuwa kwenye sehemu moja tu ya sanaa (aliwagusa Bongo Movie kwa kiasi kikubwa) Tutachukua mazuri yote ya Ruge tutakwenda nayo, asante Ruge” Steven Nyerere.

“Kama watoto wamsubiriavyo Baba nyumbani, ndivyo tulivyokuwa tukimsubiri Ruge kila jioni pale THT. Kwa miaka 15, hajawahi kuacha kuja”-Lameck Ditto.

Nguvu za kusimama hana, bado anatafariki mshumaa kuzimika mapema, Taifa linasononeka.

Wakazi wa Bukoba wamejitokeza kwa wingi uwanja wa #Gymkhana ili kuhakikisha tunamuaga salama mpendwa wetu.

Viongozi mbalimbali wa serikali wakiwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa CMG Joseph Kusaga wakiwa hapa viwanja vya #Gymkhana katika ibada ya mwisho ya mpendwa wetu Ruge Mutahaba.

“Upendo, uthubutu na kujiamini zilikuwa ni tunu zilizomsaidia kufanya aliyofanya…amefanya mengi na kugusa mengi” Waziri Kairuki.

Waziri Kairuki amesema Serikali inasikitika kwamba kifo cha #RugeMutahaba kimetokea katika wakati ambapo moto wa uchumi wa viwanda na fursa za kibiashara umekolea katika nchi yetu wakati yeye alikuwa mwanga na dira ya wengi katika kuziendea Fursa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here