Home Kitaifa Ruge alivyoisimamisha Dar

Ruge alivyoisimamisha Dar

2555
0

Karibu nyumbani shujaa, karibu nyumbani Boss, #RugeMutahaba, tuko hapa.

Tunapita njia ya Buguruni kisha kufuata njia tuliyotangaza.

Mwili wa mpendwa wetu Ruge Mutahaba, tayari umewasili katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere.

Tunapita njia ya Buguruni kisha kufuata njia tuliyotangaza.

Boss mpaka ile #MalkiaWaNguvu ya mwaka 2018 ulikuwepo, kipindi kifupi baada ya pale ulipotea ofisini. Tukaambiwa unapumzika kidogo, mara tukaambiwa unaumwa laki bado ulisema utakuja tena Ofisini.

Baada ya kutoka India ulikuja siku moja ofisini japo kwa kujikongoja, ukatusalimia na kutukumbatia ukisema “NIKO SAWA, NAHITAJI KUPUMZIKA KIDOGO TU”. Ukaenda Afrika Kusini……..hivi ndivyo unarudi?. Sawa. #PumzikaRuge

Boss, Mtaa unakulilia. Boss, umetuweza.

#RememberingRuge #JasiriMuongozaNjia

Mitaa inaita jina lako, Rugeeee, Rugee Rugeeee. Lakini hutaitika, umekwenda boss.

#RememberingRuge #JasiriMuongozaNjia

Rais Ikulu anakulilia, na hata walioko kaya za chini kabisa kwenye mitaa wametanda barabarani kukulilia: boss #RugeMutahaba wewe ni wa wote.

Labda #CloudsMediaGroup ilikuwa ngumu kupokea ile kauli yako kwamba ukifa tusherehekee, tunaona mitaa imekuelewa zaidi. Wanakimbia na gari, wanakuimbia nyimbo za kishujaa, wanakaza mioyo yao wanakupa heshima unayostahili sababu wewe ni #RugeMutahaba.

Kwani #RugeMutahaba wewe ni nani?: Waungane waandishi na wachambuzi hakuna anayeweza kujibu hilo.

Tuishie kusema wewe ni zawadi ya Watanzania, tuliyopewa na Mungu mwenyewe. Mitaa imetandika kanga upite, kwa maana kazi uliyotumwa kwetu umeikamilisha vyema.

Mdogo wetu uliyebebwa, ungekutana na #RugeMutahaba angekuambia “Inuka, angaza, paa juu ya anga, zinduka, tangaza…na una yako nafasi ya kung’aa sababu wewe ni #Kipepeo.”

Ulipotoka India na kupata nafuu kidogo, ulikuja ofisini. Wengi tulikutana na wewe kwenye ‘korido’ ukatusalimia kwa kuonesha 👍🏼, (unapendaga kuweka dole gumba kwa juu ukimaanisha kila kitu ni poa), ukasema utarudi ofisini ‘soon’. Boss Ruge, leo ndio umerudi hivi?: Sisi tumekubali. Video hii ni kumbukumbu ya safari yako ya mwisho kuingia na kutoka #CloudMediaGroup. Machozi hayawezi kumaliza uchungu tulio nao.

Lakini nenda Boss pumzika.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here