Home Kitaifa “Ruge alitusaidia kupata wadhamini”-Mkurugenzi Singida Utd

“Ruge alitusaidia kupata wadhamini”-Mkurugenzi Singida Utd

2700
0

Mkurugenzi wa Singida United Festo Sanga amezungumzia jinsi Ruge alivyokuwa msaada katika kuinua michezo huku akieleza namna ambavyo Singida United ilinufaika moja kwa moja kupitia Ruge.

“Sisi kama Singida United timu yetu ilivyopanda ligi kuu, Ruge alitusapoti kwa kiwango kikubwa . Baadhi ya wadhamini Ruge ndio alituunganisha nao lakini pia alinipa elimu ya jinsi ambavyo napaswa kuzungumza na wadhamini na kuwapata.”

“Singida United tumepata pigo kubwa kwa sababu pia alitoa fursa kwamba endapo tutapata wadhamini na wanahitaji Air Time alikuwa tayari kutusapoti kupitia Clouds.”

“Tunasikitika lakini tunasherehekea maisha ya Ruge kwa sababu hakuna kijana wa kitanzania ambaye anaweza kusema tofauti na kuwa Ruge alikuwa msaada kwa vijana. Mamilioni ya watanzania walipenda kuona Ruge anaendelea kuwa hai.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here