Home Kitaifa “Ruge alishauri Kichuya asajiliwe Simba”-Try Again

“Ruge alishauri Kichuya asajiliwe Simba”-Try Again

3664
0

Aliyekuwa Kaimu Rais wa klabu ya Simba Salim Abdallah maarufu kama Try Again katika salam zake za pole baada ya kifo cha Ruge Mutahaba, amesema atamkumbuka kwa mengi lakini ikiwa ni pamoja na ushauri wake wakati wa usajili wa Shiza Ramadhani Kichuya.

Try Again amesema Ruge alimtazama Kichuya wa Mtibwa kama star wa baadaye wa Simba na angeuzwa kwenda klabu nyingine kubwa mambo ambaye baada ya Kichuya kusajiliwa Simba yalitimia.

“Ni taarifa za kusikitisha na kuhuzunisha, si kwa wana habari tu bali kwa watanzania kwa ujumla kwa sababu Ruge ni mtu ambaye nimemfahamu kwa muda mrefu ni mtu ambaue tumekuwa tukishirikiana mambo mengi na kushauriana”-Salim Abdallah ‘Try Again’ aliyekuwa Kaimu Rais wa Simba.

“Ni mwanamichezo mwenzetu alikuwa mwanachama wetu wa Simba alikuwa anachangia timu yetu kupitia Friends of Simba lakini pia ni miongoni mwa waanzilishi wa Simba Day ambao walii-shape kufikia pale ilipofikia.”

“Ruge ni mvumbuzi ni zaidi ya kipaji, hatuwezi kumsahau Ruge katika klabu yetu ya Simba na si Simba tu bali wanamichezo kwa ujumla kwa sababu Clouds FM na Clouds TV Ruge alitufungulia milango wakati wowote tunafanya kazi na Clouds.”

“Kama ukiangalia mashindano yetu yote tunayocheza Clouds inafanya matangazo yetu kwa kina hiyo yote kwa sababu ya uhusiano mzuri tulionao kati yetu na Clouds hasa Ruge Mutahaba.”

“Kwa upande wa wanasimba tutamkumbuka sana kwa sababu alikuwa akitushauri mambo mengi. Wakati tunamsajili Kichuya tulikuwa tumekaa na Evans (Aveva) pale Protea pamoja na marehem Ruge tunajadiliana tumsajili nani kati ya Kichuya na Juma Mahadi, Ruge akashauri tumsajili Kichuya tumtengeneze awe star na kuuzika.”

“Unaweza kuona Ruge alikuwa na uwezo gani wa kufikiri mbali na ana jicho la kujua huyu ni nani. Mwaka 2000 wakati naanzisha kampuni nilimfata Ruge nikamwambia ninataka kufanya jambo hili, yeye ndiye aliyenichagulia jina la kampuni yangu ya Try Again hadi leo wanaita Try Again lakini Ruge ndio alitoa jina hilo na mpa leo limekuwa hivi.”

“Kwa niaba ya klabu yetu (Simba) natoa pole za dhati kwa wazazi na familia ya Ruge lakini pia kwa familia ya Clouds, wanahabari na wanamichezo na wasanii wote kwa ujumla.”

Klabu ya Simba imeshamuuza Kichuya kwenye klabu ya nchini Misri ambako sasa anacheza ligi kuu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here