Home Kimataifa Ronaldo akaribia kuinunua Real Valladolid na kuwa raisi wao

Ronaldo akaribia kuinunua Real Valladolid na kuwa raisi wao

11241
0

Ronaldo De Lima Nazario amebakisha hatua chache tu kuwa mmiliki wa klabu ya soka ya ya Real Valladolid inayoshiriki ligi kuu nchini Hispania(La Liga).

Wiki iliyopita kulikuwa na taarifa kwamba nyota huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil anakaribia kuwa mmiliki mkuu wa hisa katika klabu hiyo ya Valladolid.

Lakini hapo jana gazeti maarufu la nchini Hispania la Marca limetoa taarifa kwamba Valladolid wanakaribia kukubali kiasi cha Euro 30m ambazo Ronaldo anataka kuwapa Valladolid.

Kama Ronaldo atafanikiwa katika hili baasi atakuwa raisi wa klabu hii huku Carlos Suarez ataendelea kuwa kiongozi ndani ya timu hiyo lakini atabadilishiwa nafasi.

Ronaldo aliwahi kushinda kombe la dunia 2002 akaipeleka fainali kombe la dunia 1998, lakini pia ni mchezaji bora wa FIFA 1996, 1997 na 2002.

Kama Ronaldo atafanikiwa hatakuwa mchezaji wa kwanza kumiliki klabu kwani tayari David Beckham anaimiliki Miami Mls lakini vile vile Didier Drogba ana share Phone Raising.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here