Home Ligi BUNDESLIGA Roman Abromovich aingia mwenyewe sokoni, nyota hawa kutua Chelsea hivi karibuni

Roman Abromovich aingia mwenyewe sokoni, nyota hawa kutua Chelsea hivi karibuni

16373
0

Siku za hivi karibuni Manchester City pamoja na Manchester United wanaonekana kutawala sana soko la usajili na sasa Liverpool nao wanaonekana kutumia sana pesa.

Chelsea wamekuwa hawana mbwembe sana katika siku za usoni na hata sajili zao mara nyingi zimeonekana za kawaida tofauti na wenzao na hii inaweza kuwa chanzo kwa wao kutofanya vizuri msimu uliopita.

Lakini sasa baada ya kumchukua Maurizio Sarri kama kocha wao mpya, inaonekana tajiri wa Chelsea Roman Abromovich amepania kurudisha heshima katika klabu hiyo.

Kwanza Abromovich anatajwa mwenyewe kuingilia uhamisho wa Gonzalo Higuain kutoka Juventus, na Sarri anataka nyota huyo awepo katika kikosi chake cha msimu ujao.

Abromovich tayari ameshawasiliana na wawakilishi wa Ac Milan mwishoni mwa wiki kwa ajili ya usajili wa Gonzalo Higuain ambaye ada yake inatajwa kuwa zaidi ya £55m.

Ujio wa Higuain Chelsea unaweza kuamua hatma ya Alvaro Morata katika kikosi hicho, Morata amekuwa akikosa nafasi ya kudumu ndani ya Chelsea na kama Higuain akitua Chelsea inaweza kumuondoa kabisa Stamford.

Kocha Maurizio Sarri amekiri kwamba hatma ya Morata inabidi apate muda kumuangalia lakini akaweka wazi kwamba katika mechi yao ya kwanza dhidi ya Perth Glory nyota huyo alicheza chini ya kiwango.

Wakati habari za kumtaka Higuain hazijaisha ,inasemekana Abromovich alikutana na Marina Granovaskaia wakala wa nyota wa Borussia Dortmund Christian Pulisic wikiendi iliyopita.

Kumbuka kwamba Pulisic yupo pia katika rada za Real Madrid na PSG lakini Abromovich yuko tayari kutoa kitita cha £65m ili kumleta Pulisic Stamford Bridge katika msimu ujao.

Wakati Chelsea wakiwa wanajitahidi kujenga kikosi chao, upande wa pili inasemekana Barcelona na Real Madrid bado zimeing’ang’ania Chelsea na kutaka kuwanunua nyota wao.

Leo kulikuwa na tetesi kwamba Real Madrid imetuma ofa ya £100m kuwanunua Courtois na Willian(Chelsea hawajathibitisha) lakini Barca nao wanamtaka Willian, huku Real Madrid bado wakijiandaa kutuma ofa kubwa kwa ajili ya Eden Hazard.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here