Home Kimataifa Rodrygo ana vitu vitatu “Kipaji cha Neymar, kivuli cha Pele na nyayo...

Rodrygo ana vitu vitatu “Kipaji cha Neymar, kivuli cha Pele na nyayo za Robinho”

13610
0

Amezaliwa kule Osasco, katika jiji la São Paulo. Sasa hivi ukiachilia mbali dili la Vinicious kujiunga na Madrid basi kuna mtu anaitwa Rodrygo. Rodrygo alijiunga na Santos’ akiwa na mika 10 mwaka 2011. Mwezi mach 2017 alipata nafasi kuitwa kwenye kikosi cha wakubwa akiwa na miaka 16, kule nchini Peru aliposhiriki Copa Libertadores kwenye mechi dhidi ya Sporting Cristal. Kocha Dorival Júnior ndiye aliyempa nafasi ya kuonesha uwezo wake.

Rodrygo Goes ni jina liliotawala sana kwenye soka la Brazil maarufu kama “Paulista football”. Santos imekuwa kisima cha vipaji. Ana miaka 17 na tayari Santos imemkabidhi jezi namba 9.

Jina kubwa la mwisho Santos ni Neymar kwa sasa Rodrygo anaonekana kutajwa tajwa sana kama mrithi sahihi wa Neymar hasa kutokana na uwezo wake. Huyu Rodrygo amechanganya Uneymar ndani pia ana urojo wa Urobinho. Neymar aliisaidia Santos kushinda Copa Libertadores mwaka 2011, na makombe mengine mengi kabla ya kujiunga na miamba ya FC Barcelona mwaka 2013. Neymar aliifungia Santos mabao 136 kwenye michezo 224.

Tarehe 21 Julai 2017, Rodrygo ndipo alipofanikiwa kumwaga wino kwa mara ya kwanza. Aliweka kandarasi ya miaka mitano na ilipofika 1 Novemba akapandishwa kikosi cha wakubwa na aliyekuwa kocha wa muda Elano.

Rodrygo ameanzia maisha yake pale Santos akiwa na akapelekwa timu ya wakubwa ndani ya Vila Belmiro (Uwanja wa Santos). Belmerio ndio sehemu ambayo Pele alimalizia maisha yake ya soka. Na ndio sehemu pekee Pele alipofanyia maajabu makubwa. Pele pia alipata nafasi ya kuichezea Santos akiwa na umri wa miaka 16 pekee sawa na Rodrygo. Msimu wa kwanza wa Pelé alifunga mabao 36 kwenye michezo 29 pekee. Msimu uliofuata alifanya maajabu makubwa zaidi kwa kufunga mabao 58 kwenye michezo 38.

Mastaa wengine waliozaliwa pale Vila Belmerio ni watu kama Coutinho, Pepe, Giovanni, Pitta, Robinho, Diego, Neymar na Paulo Henrique Ganso ni moja ya magwiji wa soka walioacha heshima kubwa hapa Vila Belmiro. Pelé alifanya maajabu sana mnamo Novemba 21, 1964, ndani ya Vila Belmiro, alipofunga mabao 8 dhidi ya Botafogo (SP), huku Santos ikiizika Botafogo SP kwa mabao 11. Rodrugo nae akiwa na U-17, alifunga mabao 24 kwenye michezo 22. Kwenye ushindi wa kihistoria wa mabao 15-0 dhidi ya Jabaquara, alitupia 6.

Rodrygo wakati anajiunga pale Alvinegro akiwa na miaka 9 alionesha uwezo wa hali ya juu. Hata mimi binafsi nimeona baadhi ya video zinaonesha uwezo wake. Bila shaka huyu ndiye mrithi halali wa Neymar au Robinho. Ukitaka kujua maji hufuata mkondo akiwa na miaka 11 aliweka rekodi ya kuwa mchezaji mchanga zaidi kupata udhamini wa Nike kabla ya Shane Kluivert, mtoto wa Patrick, kupata udhamini huo akiwa na miaka 9 tu.

Rodrygo alicheza mchezo wake wa kwa za ndani ya SERIE A mnamo 4 Novemba 2017 siku tatu baada ya kupandishwa kikosi cha wakubwa. Alichukua nafasi ya Bruno Henrique akiishuhudia timu yake ikishindilia mabao 3–1 dhidi ya Atlético Mineiro.

Tarehe 25 Januari alifunga bao lake la kwanza 2–1 Ponte Preta. Klabu hii ya Ponte Preta ilikuwa klabu ya mwisho kabisa Pele kucheza dhidi yake katika mechi za mashindano ndani ya Brazil. Mnamo Oktoba 2, 1974, Pelé alicheza mchezo wake wa mwisho kwa Santos dhidi Ponte Preta walipoitwanga mabao 2–0 hata hivyo Pele aliondoka uwanjani kabla mchezo kuisha huku akilia kwa uchungu mkubwa.

Rodrygo alicheza kombe la Copa Libertadores mnamo 1 Machi 2018, akichukua nafasi ya Eduardo Sasha walipopoteza ugenini kwa mabao 2–0 dhidi ya Real Garcilaso akiwa na umri wa miaka 17 na siku 50 na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji pekee wa Santos mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kucheza katika michuano hiyo. Siku 15 baadae alifanikiwa kufunga bao lake la kwanza katika michuano hiyo katika ushindi wa mabao matatu 3–1 dhidi ya Nacional kwenye uwanja wa Pacaembu Stadium akiwa na umri wa miaka 17 na miezi miwili na siku 6 na kuwa mchezaji mdogo zaidi katika historia ya Brazil kufunga bao kayika michuano hiyo.

Los Blancos inasemekana wameweka Kitita cha €45 million kwa ajili ya kijana huyu mdogo anayetarajiwa kuvaa mikoba ya Neymar na Pele. Akiwa na 17 tu tayari Real Madrid wameshaanza kummendea kwa dau nono ili kufuata nyayo za Robinho. Inasemekana ifikapo 2019 huyu atakuwa mali halali ya Madrid.. Mjukuu huyu wa Pele kisoka anatarajia kujiunga na Madrid atakapofikisha umri wa miaka 18 ambayo ndio unaruhusiwa kwa mwanandinga kusakata kabumbu nje ya taifa lake.

Ndani ya michezo 23 amefunga mabao 9 akiwa na miaka 16 tu. Wakala wa Rodrygo Aguri amethibitisha kuwa Rodrygo atasaini kandarasi ya miaka 6 na Real ambapo atadumu na mafahali hao wa ulaya mpaka ifikapo 2025. Atakuwa amefuata nyayo za Robinho ambaye pia aliwahi kujiunga na miamba hao

Privaldinho (instagram) usisahau pia kufuatilia youtube Channel yetu ya Dauda Tv.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here