Home Ligi BUNDESLIGA Ribery amwaga wino, James siondoki ng’oo

Ribery amwaga wino, James siondoki ng’oo

7630
0

Mshambuaji wa klabu ya Bayern munch, Frank Ribery, ameongeza mkataba mwaka wa mwaka moja na klabu hiyo utakao mfanya abaki klabuni hapo mpaka mwaka 2019, mshambhuliaji huyu mwenye umri wa miaka 35, mkataba wake wa hapo awali ulikuwa unafikia tamati mwisho wa msimu huu.

Ribery,mpaka sasa katika katika klabu hiyo amechezea michezo 305 katika mashindano yote na kufunga mabao 179,katika ligi kuu ya Ujerumani,amecheza michezo 247, na kufunga mabao 80 mpaka sasa.

Mpaka sasa, mchezaji huyo ametwaa makombe 15 kwa ngazi ya klabu .

Ametwaa kombe la ligi kuu ujerumani, maarufu kama bundesliga mara 8 , mwaka 2007/08, 2009/10, 2012/2013, 2013/2014, 2014/15, 2015/2016,2016/2017, na 2017/18,

Pia ametwaa kombe la uefa Mara moja mwaka 2012/13, ametwaa kombe la ujerumani mara 4 mwaka 2010/11, 2012/2013, 2016/17, 2017/18.

Pia ametwaa klabu bingwa ya dunia mara 1 mwaka 2014, mwaka 2012/13, alishinda tuzo ya mchezaji bora wa uefa.

Taarifa na Aziz Mtambo

Rodriguez Anahitaji Kuendelea Kubakia Bayern Munich

MCHEZAJI James Rodriguez, anayecheza katika klabu ya Bayern Munich ameeleza kwamba bado anahitaji kuendelea kuwa mchezaji wa klabu hiyo kwa muda mrefu zaidi.

Rodriguez ambaye anachezea katika klabu hiyo ya Ujerumani kwa mkataba wa mkopo akitokea klabu ya Real Madrid. Alisema kwamba matarajio yake bado yapo Bayern, hivyo anahitaji uhamisho wa kudumu.

Ifahamike kwamba nyota huyo wa Colombia anatarajia kumaliza mkataba wake wa mkopo mwishoni mwa msimu ujao katika klabu ya Bayern.

Mwenyekiti wa Bayern Karl-Heinz Rummenigge alithibitisha mwishoni mwa mwezi huu kwamba, wana fursa ya kumsainisha Rodriguez mkataba wa kudumu kulingana na uhodari wake ambao umekuwa msaada kwa timu.

“Ligi ya Ujerumani ni nzuri sana, na furahia kuwepo hapa. Nimekuja hapa kwa mtazamo tofauti.

“Najisikia vizuri sana, natumaini nitakuwa hapa muda mrefu zaidi,”alisema Rodriguez baada ya kumalizika mchezo wao na Cologne.

Habari na Daniel S fute

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here