Home Ligi EPL Rekodi zilizowekwa EPL hii leo, Milner amkuta David Beckham huku Mendy akimkuta...

Rekodi zilizowekwa EPL hii leo, Milner amkuta David Beckham huku Mendy akimkuta Nasri

9957
0

Brighton 2 Fulham 2. Kwa mara ya kwanza tangu 2014, Andre Schurle amefanikiwa kufunga mechi mbili mfululizo katika ligi kuu ya Uingereza EPL.

Aleksandar Mitrovick aliifungia bao la pili Fulham, tangu mwezi February hadi sasa hakuna mchezaji ambaye amewahi kufunga mabao mengi EPL kama yeye(16).

Glen Murray aliifungia goli Brighton kwa penati na sasa ni Mo Salah(13), Sergio Aguero (12) ndio ambao wamefunga mabao mengi kuliko yeye katika viwanja vya nyumbani 2018.

Crystal Palace 0 Southampton 2. Ukiacha goli la Pierre Hojbjerg, Danny Ings alifunga lingine kwa Southampton na kumfanya kufunga katika michezo mitatu mfululizo ya ugenini ya Southampton.

Chelsea 2 Bournemouth 0. Katika michezo 23 hapo kabla Pedro alifunga mabao 2 tu lakini msimu huu katika mecho 4 tu amefunga mara 3 baada ya leo kufunga bao moja la Chelsea.

West Ham 0 Wolverhampton 1. Kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu ya West Ham huu ndio msimu ambao wamepoteza michezo minne mfululizo ya mwanzo katika ligi.

Leicester City 1 Liverpool 2. Sadio Mane aliwafunga Leicester kwa mara nyingine na sasa anakuwa amehusika katika magoli 4 dhidi yao katika mecho 4 alizokutana nao (goli 2, assist 2).

Roberto Firmino alifunga bao lingine kwa Liverpool ikiwa assist ya James Milner na sasa Milner anakuwa na assist 80 EPL sawa na nyota wa zamani wa United David Beckham.

Man City 2 Newcastle 1.Kwa mara ya kwanza tangu ajiunge na Man City, Kyle Walker hii leo amefanikiwa kuifungia Man Citu bao la kwanza, hili limekuja baada ya michezo 52.

Benjamin aliassist bao la Raheem Sterling na sasa anakuwa mchezaji wa pili kuwahi kutoa assists 4 katika michezo 4 ya mwanzo ya ligi kwa Man City baada ya Raheem Sterling 2015/2016.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here