Home Kitaifa Rekodi ya Mbao inaitesa Yanga Mwanza

Rekodi ya Mbao inaitesa Yanga Mwanza

3117
0

Yanga leo inaingia uwanja wa CCM Kirumba Mwanza kujaribu kufuta rekodi mbaya ya kuchapwa mechi zote na Mbao FC kwenye uwanja huo. Kwa ufupi Mbao imeshinda mechi zote dhidi ya Yanga kwenye uwanja wa Kirumba.

Mbao imeshinda mechi zake zote za ligi ilizocheza na Yanga kwenye uwanja huo pamoja na mmchezo mmoja wa nusu fainali ya FA Cup ambapo Mbao iliifunga Yanga na kufuzu fainali.

Kocha wa Yanga Zahera Mwinyi amesema siku hazifanani, matokeo yaliyopita tayari ni historia na Yanga haiwezi kufungwa kila siku na Mbao.

Mbao inaingia kwenyemchezo huo ikiwa na kumbukumbu nzuri ya kuifunga Simba kwenye uwanja wa Kirumba msimu huu, ikiwa ndio timu pekee iliyoifunga Simba kwenye ligi.

Yanga imetoka kupoteza mchezo uliopita kwa kufungwa 1-0 na Simba na inatambua kupoteza mchezo wa leo itakuwa ni faida kubwa kwa wapinzani wake (Azam na Simba) kwenye mbio za ubingwa wa ligi.

Tayari Yanga imecheza mechi 24 na kuvuna pointi 58 ikiwa inaongoza ligi wakati Mbao yenyewe ipo nafasi ya 6 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 36 baada ya kucheza mechi 26.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here