Home Kimataifa Rais wa CAF apangua tuhuma zinazomkabili

Rais wa CAF apangua tuhuma zinazomkabili

2819
0

Rais wa CAF Ahmad Ahmad kwa mara ya kwanza amejibu tuhuma za Mussa Bility wakati akiwa kwenye michuano ya Afrika kwa vijana chini ya miaka 20 ambayo ilikuwa inafanyika Niger.

Alipata fursa ya kuzungumzia mambo kadha wa kadha ikiwemo tuhuma zilizokuwa zinaelekezwa kwake na mmoja kati ya wajumbe wa kamati ya utendaji ya CAF Musa Bilitti ambaye ni raia wa Liberia.

Bility alikuwa akimtuhumu Ahmad Ahmad kwamba amezipa nchi uenyeji wa mashindano ya AFCON akikumbushia Cameroon, Ivory Coast na Guinea akidai ilikuwa ni kwa utashi wa Ahmad Ahmad.

Ahmad Ahmad anasema, akimtuhumu yeye kama Rais hamtendei haki kwa sababu maamuzi ni ya kamati ya utendaji ambayo inawajumbe 23 na yeye (Bility) akiwa ni kinara wa kamati ya utendaji.

Kamati ya utendaji ina watu 23 lakini anayemtuhumu ni yeye pekeyake watu wengine wapo kimya na mambo yanakwenda.

Shutuma nyingine ambayo ameizungumzia ni kuhusu kufanya makubaliano na kutoa deals kwa baadhi ya makampuni pasipo kamati ya utendaji kuwa na taarifa.

Ahmad Ahmad amesema kwa mujibu wa katiba ya CAF kamati ya utendaji inavikao viwili kwa mwaka lakini katiba ya CAF inamruhusu Rais kuitisha vikao vingine vya dharura.

Kwa hiyo kutokana na kipengele hicho katika utawala wake pamoja na katiba kuzungumzia vikao viwili vya kamati ya utendaji yeye amekuwa akiitisha vikao vitatu hadi vinne na anayoyasema hayo yote yamekuwa yakijadiliwa kwenye kamati ya utendaji.

Lakini pia kuna kamati za dharura kwa mujibu wa katiba ya CAF inaweza kukaa kushughulikia na kufanya maamuzi kwa hiyo kama Bility hakuwa sehemu ya mikutano hiyo ya kamati ya utendaji asituhumu kwamba kamati ya utendaji imerukwa, taratibu zote zilifuatwa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here