Home Kitaifa Rabbin Sanga anandoto ya kufanya makubwa Ulaya

Rabbin Sanga anandoto ya kufanya makubwa Ulaya

2947
0

Ikiwa ni siku ya nne kwa Rabbin Sanga nchini Uturuki, nyota huyo wa mashindano ya Ndondo Cup Academy anaendelea na majaribio yake kwenye academy ya Besiktas.

Pamoja na majaribio hayo, lakini mambo mengine yanaendelea nje ya majaribio yake na amekuwa akitembelea vivutio mbalimbali. Leo amepata fursa ya kutembelea uwanja wa timu ya Besiktas unaojulikana kwa jina la Vodafone Park.

Sanga amepata fursa ya kuangalia namna klabu hiyo inavyofanya shughuli zake mbalimbali pamoja na kutembelea duka lao kubwa wanapouza bidhaa mbalimbali zikiwemo jezi, nguo za aina mbalimbali na vitu vingine kibao.

Ametembelea pia makumbusho na kujifunza vitu mbalimbali, vyumba vya kubadilishia nguo, ukumbi wa mikutano na waandishi wa habari, sehemu ya chakula, sehemu ya play station n.k.

“Kwangu ni faraja kubwa, ni uwanja wa kwanza kwangu kuuona unaochezewa mechi kubwa hapa barani Ulaya, nimeona vitu vingi ambavyo ni mara ya kwanza kwangu.”

“Nimependa wenzetu wanavyotunza vitu vyao kwa ajili ya kumbukumbu nimeona sehemu wanatunzia makombe yao kwetu hakuna vitu kama hivi.”

“Natamani siku moja nicheze kwenye uwanja huu nikiwa na timuu hii (Besiktas) au timu nyingine ya Ulaya.”

Safari ya Sanga imewezeshwa na kampuni ya Beko inayotengeneza na kuuza vifaa vya umeme vya nyumbani (friji, pasi, Tv, mashine za kufulia)

Rabbin Sanga anasema akirudi uwanja wa Besiktas anataka kucheza na sio kutalii tena, angalia video #YouTube kupitia #DaudaTV uone jinsi dogo huyu alivyokuwa na ndoto kubwa kwenye soka. Bofya PLAY▶hapa chini 👇

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here