Home Uncategorized Pogba siwezi kumsahau Abou Diaby

Pogba siwezi kumsahau Abou Diaby

5559
0

Hivi unamkumbuka vizuri Diaby? Yule fundi wa kukokota mpira? Jamaa aliheshimika sana kwa uwezo wake wa kutembea mpira kutoka tegeta mpaka Chamazi. Wengi walimwita box to box.


Takwimu za Diaby

Mechi -201 ngazi za vilabu

Timu ya taifa – Mechi 16


Shida yake ilikuwa moja tu, BISKUTI. Hakuwahi kuwa na amani kabisa na miguu yake. Alibarikiwa chenga nguvu, akili na ufundi vyote vya kiutu uzima lakini akapewa miguu ya mtoto mdogo (Milaini).

Abou Diaby baada ya safari ndefu yenye mabonde mengi sana katika soka lake amekubali yaishe.

Ameamua kuachana na soka, huku akiacha gumzo kubwa sana la kusumbuliwa sana na majeraha.


Alipokuwa Arsenal alikaa njee siku 1554 katika Kipindi cha miaka 9 ambapo ni sawa na wiki 222 (miaka 4)


Nyota wa United na bingwa wa kombe la dunia Paul Pogba amesema yeye hawezi kabisa kumsahau Diaby.

Pogba aliwahi kuwataja viungo bora duniani ambao yeye ana amini kuwa wamemzidi uwezo na anajifunza menfi kupitia wao ni Iniest, Kroos, Modric, Toure, Debruyne na Mr Aboud Diaby

“Nimejifunza mengi kutoka kwake. Naheshimu sana kipaji chake. Hata timu ya taifa alikuwa na kipaji cha hali ya juu” Pogba

Diaby alianza maisha yake ya soka 2004 pale Auxerre na amefanikiwa kucheza takribani mechi 214 kwenye ngazi ya vilabu na mechi 16 timu ya taifa.


Alipotua Arsenal, Arsenal ilicheza michezo 350 yeye alifanikiwa kucheza michezo 124 tu.


Diaby alijiinga na Marseille ya Ufaransa ambapo msimi wa 2016-17 alicheza mechi mbili tu na zote alitoka dakika ya 61, 60.

Mnamo 21 mwezi wa 8 mwaka 2016 Daiby aliumia enka. Akafanyiwa operesheni.

Alikaa nje kwa muda wa miezi takribani 6. Aliporudi aliwaomba Marseilles wampe likizo.

Aliomba likizo ya mwaka mmoja kwa lengo ya kuipa muda misuli yake ipoe. Yaani kibongo bongo alikuwa anaizugisha misuli yake ili akirudi aanze upyaaaa.


Katika historia ya maisha yake akiwa ameumia mara 44


Mwisho wa siku alijikuta amekaa miaka miwili na bado misuli yake ikawa inamsumbua. Mwisho akasema kwani shilingi ngapi? Akabwanga manyanga.

Kila la kheri kwake katika maisha mapya.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here