Home Ligi EPL Picha la Mourinho na Martial lachukua sura mpya, Martial amchana “Special One”

Picha la Mourinho na Martial lachukua sura mpya, Martial amchana “Special One”

16460
0

Baada ya kimya cha takribani siku saba hatimaye Anthony Martial amefunguka na kuweka hadharani ni nini kinaendelea katika maisha yake ya sasa na kuhusu Manchester United.Tangu mwisho mwa wiki iliyopita baada ya Martial kurudi Ufaransa kwa ajili ya kuntizama mkewe aliyetarajia kujifungua, mengi yalizungumzwa na wengi walikuwa wakisema yao.Kuna waliosema kwa Martial aliondoka kambini kwa kulazimisha na Mou akamruhusu kishingo upande, na huku wengine wakisema Mourinho amepanga kumuadhibu Martial akirudi.Wakati yote hayo yakiendelea, upande wa Athony Martial ulikuwa kimya lakini hii leo Martial ameeleza kuhusu jambo hili na kwanza amesema familia yake na mtoto wake mpya wanaendelea vizuri.Kupitia account yake ya Twitter Mfaransa huyo pia amesema kwamba kuhusu suala la timu na familia mara zote kwake hakuna kilicho juu ya familia (ni familia kwanza baadae mambo mengine yanafuata).Kauli hii imetafsiriwa jama jibu kwa Jose Mourinho ambaye alisikitishwa na kitendo cha Martial kurudi Ufaransa na kuakaa jwa muda mrefu wakati timu iko katika maandalizi ya msimu mpya.Tweet ya leo ya Martial inaweza kuchochea ugomvi wa chinichini kati yake na Mourinho, na kwa kariba ya kocha kama Jose Mourinho inaweza ikamfanya Martial kuchungulia mlango wa kutokea Old Traford.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here