Home Kitaifa Paulo kumbuka ata “Kessy” Aliwahi kucheza Yanga

Paulo kumbuka ata “Kessy” Aliwahi kucheza Yanga

5597
0

Wakati naanza kidato cha tano kwenye shule ya sekondari Kishoju iliopo wilayani Muleba mkoani Kagera nilishangaa sana kuona aina moja ya pikipiki kutumika sana zikienda kwa jina la Boxer, Baada ya hapo ilibidi nilifuatilie suala hii kiundani kwanini ni aina moja tu ya pikipiki inayotumika zaidi mkoani kagera baada ya mda nikapata jibu kumbe ni kijiografia zaidi yaani kutokana na uasilia wa mazingira kua na milima mingi kwahiyo pikipiki aina hiyo zinauwezo mkubwa kwenye kupandisha hiyo milima.

Paulo Godfrey “Boxer” ni beki wa kulia wa timu ya wananchi Dar es salaam Young Africans na amekua na kiwango kizuri na kutengeneza ukuta mgumu upande wa kulia wa yanga kiasi kwamba kustahili kupewa jina la “Boxer ” akilinganishwa na uwezo wa aina tajwa ya pikipiki, nimemfuatilia siku nyingi hivi sasa kiasi kwamba kuona Kuna kitu kipya ndani ake ambapo akipata msimamizi na mushauri mzuri natarajia kumuona mbali zaidi katika misimu mitatu ijayo. Binafsi nilimuona akifanya vizuri kwenye mechi za kawaida nikahisi anaweza asiweze kustahimili joto la mechi ya watani wajadi lakini mechi ya iliopita ya mzunguko wa pili dhidi ya watani wao wa jadi Simba sports club iliyoisha kwa kulala kwa bao moja kwa bila lililofungwa na Merdie Kagere “Paulo” alifanikiwa kucheza vizuri kiasi kwamba kumpoteza mshambuliaji tishio wa Simba Mganda Emanuel Okwi.

Paulo amekua na uwiano mzuri kwenye kujilinda na kuanzisha mashambulizi dhidi ya timu pinzani ambapo upande wa kulia wa yanga umekua mgumu zaidi na upande unaotumika zaidi katika kuleta matokeo chanya kwa club hiyo inayonolewa na mkongomani Papa Mwinyi Zahera. Kitu pekee cha kumuasa Paulo ni kuzidisha nidhamu ya kimichezo, kufanya mazoezi kwa kujituma na akumbuke ata Hassan Kessy aliwahi kupitia yanga na Leo yupo Nkana ya Zambia

by Raphael Lucas
0764764449/0710690782

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here