Home Kimataifa Paul Merson awatolea uvivu Arsenal na kuihofia United.

Paul Merson awatolea uvivu Arsenal na kuihofia United.

2662
0

Mmoja kati ya wachambuzi hodari wa soka barani Ulaya Paul Merson amesema viongozi wengi wa Arsenal wana mipango mifupi na isiyo na tija.

“Naifahamu Arsenal nje ndani. Kwa miaka 10,11 mpaka 13 wamekuwa wakipigania kuingia top four”

“Kwa United hilo ni jambo la ajabu sana kujadiliwa na viongozi. Nakubali wameyumba hivi karibuni lakini sio wa kuwabeza hata kidogo”

“Ni ndoto za mchana kusikia Arsenal wanajipanga kutwaa ubingwa. Wataanza vipi? Watampa mkufunzi jukumu la top four”

“Wakifanya vizuri mechi kadhaa watahamisha mawazo yao kunyakua ubingwa. Baada ya mechi 10 wakifanya vibaya watanyamaza. Hovyo kabisa”

“Man United msimu huu nakubali hawana mpango wa ubingwa lakini wanapigania top four. Lakini msimu ujayo watalenga kunyakua ubingwa. Watasajili majina makubwa. Wataongeza wachezaji mishahara.”

“Mipango yao utaiona. Wala hutasikia malalamiko ya wachezaji. Mabosi watajitoa kuhakikisha wanamsapoti mkufunzi lakini sio Arsenal.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here