Home Entertainment Orodha ya wachezaji waliowahi kushare wapenzi, Cristiano Ronaldo ndio kinara wao

Orodha ya wachezaji waliowahi kushare wapenzi, Cristiano Ronaldo ndio kinara wao

16484
0

Wacheza soka wengi ni vijana na maisha ya umaarufu mara nyingi yanakumbana na story nyingi sana, leo nataka nikupe nyota wakubwa wa soka ambao wamewahi kudate na mwanamke mmoja.

Cristiano Ronaldo & Sergio Ramos(Nareida Gallardo). Mwaka 2007 mwanamitindo Gallardo alikutana na Ramos katika club usiku na hapo mapenzi yao yakaanza lakini miaka miwili baadae akakutana tena na Cr7 pia wakaanzisha mahusiano, japo baadae Gallardo alimwagwa na nyota hao wawili.

Cr7 kwa sababu ambazo hazikuwekwa wazi aliamua kummwaga Gallardo kwa ujumbe mfupi wa message na mwanadada huyo akaona ngoja nimuoneshe huyu Mreno, alikwenda kwenye Tv na kusema Cr7 ni goi goi katika mambo ya watu wazima.

Mario Balotelli & Cristiano Ronaldo(Rafaella Fico). Ronaldo tena huyu hapa kwa Rafaella na inasemekana(Rafaella alisema) Ronaldo alikuwa mwanaume wa kwanza kuwahi kutoka naye kimapenzi lakini kama ilivyo Gallardo huyu naye alimponda Cr7 kwa mambo ya chumbanj kuwa ni goi goi.

Mwaka 2011 Rafaella akaanza kutika na Mario Balotelli katika uhusiano ambao haukuzidi hata miezi 5, baada ya wawili hao kumwagan Rafaella alidai ana mimba ya Balotelli lakini mshambuliaji huyo wa Italia aliikataa hadi baadae vipimo vga DNA vilipothibitisha kuwa ni kweli.

Cristiano Ronaldo & Marcus Bent(Gemma Atinkson). Ronaldo tena huyu hapa, na Gemma alimnasa Ronaldo tangu 2007 lakini uhusiano wa hawa wawili ulivunjika baada ya muda mfupi japo Gemma yeye hakuweka siri za chumbani za Cr7.

Baada ya mahusiano yao kuvunjika, mrembo huyu alihamia kwa mshambuliaji wa zamani wa Everton Marcus Bent, wawili hawa walipendana hadi wakachumbiana lakini uchumba wao ukavunjika ndani ya miezi miwili.

Wayne Rooney & Mario Balotelli(Jenny Thompson). Kama unakumbuka dada huyu alikuwa maarufu sana wakati mke wa Rooney akiwa na mimba ya kwanza, inadaiwa wakati mkewe akilea mimba Rooney alitoka na msichana huyu ambaye anafanya kazi katika club ya usiku.

Lakini baadae Jenny alitajwa katika break up ya Mario Balotelli na Rafaella Fico kwani Balotelli alianza mahusiano ya chinichini na msichana huyo na baada ya Fico kugundua ukawa mwisho wao.

Mesut Ozil & Matteo Ferrari(Aida Yespica). Inadaiwa kwamba Yespica ndio binti mrembo zaidi kuwahi kuzaliwa Venezuela kwenye miaka kuanzia 90+, Aida alianza kutoka na nyota wa Itakia Matteo Ferrari na wakapata hadi mtoto aitwaye Aron Ferrari.

Baada ya penzi la Ferrari na Aida kufa, Mesut Ozil akaona ndio wakati wake kujiweka kwa mrembo huyo. Aida anadaiwa alikuwa chanzo cha Ozil kuuzwa na Real Madrid kwenda Arsenal kwani nyota huyo alikuwa akisafiri kila mara kwenda kumuona Aida aliyekuwa Milan nchini Italia.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here