Home Ligi BUNDESLIGA Orodha ya wachezaji waliodanganya mashabiki wao, (Henry, Nasri,..)

Orodha ya wachezaji waliodanganya mashabiki wao, (Henry, Nasri,..)

10366
0

GAEL CLICHY

Mlinzi wa zaman wa kushoto wa Arsenal alocheza pamoja na akina Kolo Toure na Emmanuel Adebayor wote hawa walijunga Man City – among other pamoja na Yaya Toure na Carlos Tevez – walijunga Manchester City mnamo mwaka 2009. Clichy mwenyewe ana kiri alikwenda Etihad Stadium kwa sababu ya njaa.

“Ukiwa mchezaji na unahitaji hela akili yako itawaza klabu kama Manchester City,” “Wachache sana eti wanacheza vilabu ili wapate jina kubwa na makombe, wengi wetu tunacheza ili kujenga maisha yetu binafsi. Hata wale wanaodumu vilabu vikubwa kwa muda mrefu wengi wao wanalipwa fedha nyingi sio kwamba eti wanavipenda hivyo vilabu. Anapokuja mtu na mshahara wa £300,000 kwa wiki daah unahisi kuchanganyikiwa. Lakini mimi siwezi kuondoka Arsenal kwa sababu ya tamaa nisharidhika”

Baada ya maneno hayo Clichy alijunga na Man City na kucuhubua ubingwa.
Maana yake kile alichokiongelea kuhusiana na tamaa.

SAMUEL ETO’O

Baada vurugu la UEFA hatua ya 16 bora kati ya Barcelona na Chelsea mwaka 2005, Eto’o alisema haitokaa itokee achezee timu ambayo inagundishwa na Jose Mourinho.

”Haiwezi kutokea mimi kufanya kazi na Mourinho,”

“Nimekerwa sana na aina yake ya tabia alizoonesha kwenye mchezo wetu dhidi yao”

Kabla ya mchezo Eto’o alisema “Ni bora niruddi kuuza karanga kijijni kwetu kuliko kuchezea timya kipuuzi na ovyo kama Chelsea”

Baada alikwaruzana na Mourinho na akatoa maneno ya kashafa kwa kusema “Mwanzoni nilijua Mourinho ni kocha mkubwa kumbe ni mpuuzi tu”

Wanakwambia kabla hujaropoka hakikisha hakuna waandishi wa habari pembeni.

Eto’o akasajiliwa na Mourinho yule yule kwenda Inter mwaka 2009 na kushinda makombe matatu na kuweka historia katika klabu ile kabla ya kujiunga nae tena Chelsea mwaka 2013. Wanakwambia mbwa usiyeishi nae usimpige jiwe ipo siku anaweza kuwafukuza wezi wanaotaka kuvunja nyumba yako.

ALAN SMITH

Smith ni miongoni mwa wachezaji wa kihisyoria wa klabu ya Leeds. Mashabiki wengi walimsujudu sana kiasi cha kumfanya aropoke kuwa haitoweza kutoka aichezee klabu nyingine hata ije Manchester United”. Smith akiwa mtoto aliichezea Man United ya watoto na kutemwa kitendo kilichomuumiza sana. Mnamo mwaka 2004 Leeds wakashusshwa daraja na akajikuta anajiunga tena na Red Devils

Leeds walihitaji kiasi kikubwa vha hela na hakuna timy nyingine iliyoweza kutoa dau hilo zaidi ya Man United.

Miaka minne baadae alisema: “nilikuwa mjinga sana wakati ule, niliona Leeds nimerika wala sikuwahi kudhani kama ipo siku Man United itanihitaji tena. Nilihitajika na Fergie kocha mkubwa, Man United ni klabu kubwa hata ingekuwa wewe ungekataa vipi, Nikagundua mawazo yangu ya zamani yalikuwa ya kitoto tu”

“Kwanza Leed nilikuwa nawadai hela nyingi sana mwisho nikawa naomba Mungu wafilisike kabisa tu”

SAMIR NASRI

Wakati wa mchezo wa Arsenal kwenye kombe la ligi (League Cup) dhidi ya dhidi ya Birmingham City mwaka 2011, Nasri alimaliza utata uliozagaa mitandaoni kuhusu kuhama kwake akasema. “Kilichonileta Arsenal ni kubeba mataji, siwezi kuondoka bila taji lolote Arsenal,”

Arsenal wakaifunga Barcelona 2-1 duru ya kwanza ya robo fainali ya UEFA. Kikosi cha mzee Arsene Wenger kikatpoteza kwa Birmingham fainali, wakatolewa FA Cup na Manchester United na mchezo wa marudiano na Barcelona wakala sumu. Ligi kuu waksshinda michezo 2 kati ya 11 michezo iliyobakia wakamaliza wanne kwenye msimamo.

Yule yule aliyesema haondoka kabla Arsenal kubeba ubingwa akaona ni rahisi sana kwa mende kujaa kabati la Arsenal kuliko kombe akatimkia Manchester City kwa £25m.

ARTURO VIDAL

Maisha ya Vidal mjini Turin yalikuwa poa sana. Alijizolea umaarufu mkubwa na kusemekena kuwa yeye ni moja ya viungo bora duniani baada ya kushinda mayaji manne mfululizo akiwa na klabu Juventus akafanikiwa kufika fainali ya uefa na Bianconeri kwa mara ya kwanza tokea 2003.

“Hapa Turin mashabiki wananipenda sana na nawapenda pia. Familia yangu ipo huru wala hakuna shaka. Sasa hapa naondoka vipi? Kwanini niondoke? Halafu niende wapi?”

Miezi minne baadae Vidal akaomba kuuzwa Bayern Munich, kama ilivyothibitishwa na mkurugenzi wa Juventus Giuseppe Marotta.

Mats Hummels

Hummels ni mmoja kati ya wachezaji ambao wanaongea sana lakini matendo yao nao ninzero. Wakati Mario Gotze anaikimbia Borussia Dortmund kwenda Bayern Munich mwaka 2013. Alisema hivi

“Sielewei kwanini Gotze amefanya maamuzi magumu vile. Kila mtu hapa ameshtushwa. Nilishamwambia abaki hapa lakini Dortmund hapamfai. Binafsi sijaona sababu zilizomuondoa hapa BVB.”

Hummels aling’atwa na maneno yake miaka mitatu baadae alipotimkia Bayern kwa kufuata nyayo za Gotze na Robert Lewandowski. Dortmund ilipokea £30m kwa uhamisho wake.

Thierry Henry
Baada ya kufungwa na Barcelona kwemye fainali ya UEFA mwaka 2006, Taarifa nyingi zilisambaa kuwa Henry yupo mbioni kutimkia Camp Nou.

“Najua malengo yangu na Arsenal yalikuwa sawa. Tumepoteza wote sioni sababu yangu kuondoka. Nipo hapa milele. Siwezi kwenda Barcelona na sipo tayari.”

Msimu wa 2006/07 Henry akajiuna na vijana wa Frank Rijkaard Barça. Hawezi kujutia sana kwank ndani mismu mitatu alibeba ligi mara mbili na uefa moja chinia Pep Guardiola mwaka 2008/09.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here