Home Kitaifa Nyoni atakuwepo!

Nyoni atakuwepo!

3606
0

Jana Erasto Nyoni alifanya mazoezi pamoja na wachezaji wote wa Simba, kocha mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema Nyoni atakuwepo kwenye mchezo wa kesho lakini watamkosa Juuko Murdhid.

“Unajua Erasto alifanya mazoezi tangu wiki iliyopita ingawa hatukusafiri naye kwenda Algeria bado tuna muda wa kuendelea kufanya naye mazoezi, nafikiri atakuwepo.”

“Juuko hapana, hatokuwepo kwa sababu anahitaji mapumziko mpaka Jumatatu kwa hiyo kwa uhakika Juuko hatakuwepo katika timu.”

“Mechi itakuwa ngumu lakini sisi tunaendelea kujiandaa vizuri ili tushinde mechi ya Jumamosi, tunafahamu timu tunayochezanayo ni nzuri kwa sababu mechi ya kwanza hatukupata matokeo lakini tunaomba tuendelee kuwa wazima naamini tutafanya vizuri”-Easto Nyoni.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here