Home Dauda TV Nonga kaeleza sababu ya kumkoromea golikipa “Huwezi kumnong’oneza”

Nonga kaeleza sababu ya kumkoromea golikipa “Huwezi kumnong’oneza”

6179
0

Kwenye mchezo wa leo wa ligi kuu Tanzania bara Lipuli vs Simba lilionekana tukio ambalo huenda lilitafsiriwa tofauti na wadau wa soka baada ya mshambuliaji wa Lipuli Paul Nonga kuonekana akimkoromea golikipa wake Yusuph Mohamed kufuatia kutunguliwa goli kwa mkwaju wa adhabu ndogo.

Chama alimchungulia Yusuph kabla hajajipanga vyema golini baada ya kuupanga ukuta wake na kufanikiwa kufunga goli ambalo lilimuacha golikipa wa Lipuli kwenye lawama na wachezaji wake.

Baada ya mechi Paul Nonga amesema hakukuwa na tatizo lakini alikuwa anajaribu kumwelekeza mchezaji mwenzake baada ya kufanya kosa na kujikuta timu ikiadhibiwa.

Angalia video hapa chini👇kupitia YouTube ya Dauda TV uone Nonga akifafanua kilichotokea kati yake na golikipa Yusuph Mohamed. Bofya PLAY▶

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here