Home Kitaifa “Nipo tayari kufundisha Yanga bure”-Zahera

“Nipo tayari kufundisha Yanga bure”-Zahera

4153
0

Kocha wa Yanga Zahera Mwinyi amesema, fedha ambazo anazitumia kwa ajili ya klabu ya Yanga hatarajii kurudishiwa pia yupo tayari kufanya kazi bila malipo.

“Mimi nawezakufanya kazi hata miaka 10 Yanga bila kulipwa, mimi nilishacheza mpira Ulaya miaka 40 sisubiri ulinipe mshahara tayari nina maisha yangu na biashara zangu nyingi.”

“Kwangu mpira ni passion upo moyoni, sio kwa sababu nina mambo yangu mengine ndio maana nasema hivi hapana. Kwa mfano Mourinho analipwa pesa nyingi sana lakini bado anaendelea kutafuta pesa, Messi analipwa pesa nyingi anaweza kucheza bila hata kulipwa lakini kila mwaka anataka kuongezwa pesa.”

“Mimi kwangu pesa sio kitu, Mungu ametupa zinatusaidia lakini mambo mengine tunapaswa kufanya bila kuweka pesa mbele. Mungu alinisaidia kidogo na mimi naisaidia Yanga, siku wakipata pesa hata ikiwa ni miaka 10 baadaye watasema tunadeni kwa mtu fulani wanaweza kuja kunipa.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here