Home Kitaifa Ninja wa Yanga aitwa TFF kusikiliza kesi inayomkabili

Ninja wa Yanga aitwa TFF kusikiliza kesi inayomkabili

3144
0

Herman Julius kwa niaba ya Katibu Mkuu wa TFF, amemwadikia barua mchezaji wa Yanga Abdallah Shaibu ‘Ninja’ akimtaka afike ofisi za TFF kwa ajili ya kusikiliza shauri lake.

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imefungua malalamiko yako(hapo chini) mbele ya Kamati ya Nidhamu ya Shirikiksho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Huu ni wito rasmi kwako kufika mbele ya Kamati ambayo itakaa Jumapili, Februari 10, 2019 saa 4:00 asubuhi katika katika ukumbi wa Ofisi za TFF uwanja wa Karume, Ilala Dar es Salaam.

Una hiai ya kufika kutoa utetezi huo kwa mdomo, kutuma kwa maandishi, kuleta mashahidi au kutuma mwakilishi akiambatana na barua ya uwakilishi. Na mwito huu ni wito wa mwisho na uthibiisho kuwa umepata taarifa ya malalamiko haya, hivyo kamati ina haki ya kufanya maamuzi dhidi yako.

Nategemea utafika kwa muda muafaka na TFF haitahusika na gharama za shauri hili.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here