Home Entertainment Nikkiwapili apigilia msumari Mourinho kutimuliwa Man United

Nikkiwapili apigilia msumari Mourinho kutimuliwa Man United

3374
0

Yamezungumzwa mengi sana kwenye mitandao ya kijamii, vijiweni na sehemu nyingine nyingi kuhusu Mourinho kupigwa chini na Manchester United.

Nikkwapili ni shabiki ‘lialia’ wa Man United, yeye pia ametoa maoni yake kuhusu Mou kutimuliwa na amependekeza aina ya makocha ambao wanaweza kurithi nafasi hiyo na kuisaidia timu.

“Naona ni jambo sahihi kwa Mourinho kuondoka kwa sababu nikiangalia kikosi cha mwisho ambacho Sir. Alex Ferguson alichukuanacho ubingwa na hiki cha Mourinho naona bado kikosi cha Mourinho ni kikali sana lakini tuna-perform vibaya mno.”

“Huwezi kuamini hadi sasa hivi tuna pointi nusu ya zile za Liverpool hata kama timu haina kiwango kizuri lakini tupo hovyo kwa kila kitu. Hata ukiangalia namna ya uchezaji tumekuwa na Mourinho system (kujilinda) timu imekuwa haina njia mbadala.”

“Akiwa kama kocha ameshindwa kuimarisha uhusiano na baadhi ya wachezaji wake, ameshawazungumzia hovyo Alexis Sanchez, Pogba, alikuwa anamuweka benchi Martial ambaye baadaye akarudi vizuri.”

“Tunaelekea mwisho wa mzunguko wa kwanza lakini hadi sasa hivi hajapata kikosi cha kwanza anaweza kubadili wachezaji nane katika mechi mbili tofauti, sasa ikifikia hatua hiyo wachezaji wataelewana vipi?

“Naona mbinu zake zilikwama au hazikuendana na wachezaji ambao wapo Man United, acha watafute kocha mwingine tuone mabadiliko gani yatakuja.”

“Nadhani Michael Carrick anapaswa kupewa timu kwa sababu kwa siku za karibuni Manchester imepoteza falsafa kwa hiyo Carrick anaweza kurudisha falsafa ya timu na tumeona kocha mpya wa Arsenal amekuja lakini ameendeleza falsafa ya klabu mpira wanaocheza sasa hivi ndio uleule waliokuwa wakicheza kipindi cha Arsene Wenger.

“Ukiangalia Barcelona hata kocha akiondoka falsafa yao inabaki vilevile hata ukienda Liverpool wana aina yao ya uchezaji. Timu ndogo kama Stock City inatushinda, Manchester ya Ferguson ilikuwa ya wachezaji wapambanaji na kutumia mawinga wanaopiga cross watu wanafunga, haijawahi kuwa timu ya kujilinda ilikuwa timu ya kushambulia tangu mwanzo mwisho.”

“Kwa hiyo Carrick akibaki labda anaweza kumleta mtu kama Giggs wakarudisha falsafa ya Ferguson hata kama atakuja kocha mpya itakuwa vizuri kama ataendeleza falsafa ya timu.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here