Home Kitaifa Ni #MbeyaDerby Mbeya City vs Prisons

Ni #MbeyaDerby Mbeya City vs Prisons

2721
0

Ebwana leo jijini Mbeya kutakuwa na #MbeyDerby (Mbeya City vs Tanzania Prisons) mechi kama kawaida itachezwa uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine.

Miaka kadhaa iliyopita derby hii ilikuwa inalisimamisha jiji la Mbeya kwa muda lakini siku zinavyozidi kwenda inazidi kuwa derby ya kawaida.

Makocha wa timu zote mbili Ramadhani Nswanzurwimo (Mbeya City) na Adolph Rishard (Tanzania Prisons).

“Tuko sawa hakuna mchezaji yeyote ambaye anamajeruhi na tumejiandaa vizuri kwa ajili ya game dhidi ya Mbeya City”- Adolf Rishard.

“Ni mechi kubwa ambayo ni muhimu kwetu na kwa Prisons, tumejiandaa na tuko tayari tunataka kumalizia kazi tuliyoifanya raundi ya kwanza ambapo tuliwafunga 2-1 na hatutaki wapindue matokeo hayo”-Ramadhani Nswanzurimo.

Mbeya City ilishinda 2-1 kwenye mechi ya mzunguko wa kwanza wa ligi kuu Tanzania bara. Mbeya City ipo nafasi ya 12 kwenye msomamo wa ligi ikiwa na pointi 30 wakati Prisons yenyewe ipo nafasi ya 17 ikiwa na pointi 29.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here