Home DOKUMENTARI N’golo Kante “panya”; kutoka kutafuta makopo mpaka tuzo

N’golo Kante “panya”; kutoka kutafuta makopo mpaka tuzo

13041
0

Hakuna mtu aliyezaliwa bila kupitia magumu. Maisha yana njia nyingi sana. Kabla hujafika mahali unapokwenda lazima ukutane na vikwazo vingi.

Leo hii Ng’olo Kante yupo Chelsea anakula Paundi 120,000 kwa wiki, huu ni mpunga poa tu lakini amini usiamini huyu alikuwa muokota makopo. Hivi majuzi nilisikia mchezaji mmoja wa Yanga akisema kuwa yeye ametokea maisha mazuri hivyo anacheza soka kwa kujifurahisha tu wala hana malengo yoyote. Nilimdharau sana. Hata hivyo kiwango chake kimeporomoka sana maana hajui umuhimu wa soka nini.

Image result for Kante salary

Amezaliwa 29-03-1991
Mahali Paris-France
Alipokulia Rueil-Malmaison, Hauts-de-Seine
Wazazi Mr Kante Baba na Mrs Kante Mama
Asili Mali (Wahamiaji) 1980
Majina Kamili

N’Golo Kanté

Jina la Utani The rat (Panya)

Wakati Ngolo Kante anaanza maisha mambo yalikuwa magumu sana.

Image result for kante untold story

Maisha yake yaliendesha kwa kuokota makopo. Wazazi wake walikuw wahamiaji kutoka nchini ya Mali. Walikwenda ufaransa kutafuta maisha. Mambo hayakuwa mazuri sana kwao. Alipoanza maisha ya shuleni alipenda sana kucheza mpira wa rugby yaani mchezo wa raga.

Related image

Siku moja nilicheza kwa kujituma sana na mwalimu wangu alinifuata akaniambia jitahidi utafika mbali. Akaniomba nianze kucheza raga niachane na soka. Mwalimu alipenda sana jitihada zangu kasha akaamua kwenda nyumbani kuwaomba wazazi wangu kuwa nianze masuaa ya kimichezo. Baba yangu akaniuliza je nipo tayari, nikamjibu nikamwabia nataka kucheza mpira wa miguu.

Kante alikuwa mtoto wa kwanza na ndiye aliyetumia muda mwingi kupambana ili kusaidia na wazazi wke ambao walikuwa ombaomba.

Image result for Kante speak
Kijiji walichotoka Kante ni kijiji ambacho wanaoishi wengi walikuwa wafanyakazi wanafumua mitaro na kufanya usafi wa jiji. Kiujumla walikuwa wakiishi uswahilini.

Kante alikuwa anzunguka jiji zima zaidi ya kilometa 20 kutafuta makopo ambayo alikuwa akienda kuyauza ili kupata kidogo kitu. Kiujumla kazi ile haikusaidia chochote familia yao zaidi tu mzunguko wa umasikini na ufukara wa kipindukia ulibakia pale pale.

Related image

Wakati wa michuano la kombe la dunia mwaka 1998 Kante alipata hamasa nyingi mpya. Hakuwahi kubahatika kuona mchezo wowote wa kombe la dunia ila alisikia baadhi ya majina makubwa mao wengi walikuwa wahamaiaji kama yeye. Kombe lile lilimpa faida kubwa sana kimaisha kwani alikuwa mfagiaji nje ya viwanja ambapo dili lake la kuokotoa makopo lilipamba moto kwani alihakikisha anatembela kila kiwanja kuhakikisha anapata makopo ya kutosha. kutokana na kombe lile makopo yalipatikana kwa wingi

Related image

Kante anakwambia hakuna kiwanja hakwenda kufanya usafi wakati wa kombe la dunia. Mwaka ule alikuwa na miaka 7 tu. Yaani wakati mimi nikiwa naenda shule ya msingi Kingachi ndugu yangu kante alikuwa anapambana na watu wazima kuhakikisha mfuko wake unajaa makopo. leo hii mimi ndo napaswa niokote makopo ya maji atakayotupa yeye. maisha yanabadilika. Jitume wala usikate tamaa.

Wakati wa Kombe la Dunia alivutiwa sana na baadhi ya mastaa kama vile

Jina asili
Ruddy Lilian Thuram-Ulien Tunisia
Patrick Viera Senegal
Zinedine Zidane Algeria
Thiery Henry Senegal
Nicholas Anelka Algeria

Mwisho shule ilimshinda na kuamua kujiunga na klabu ndogo ya mtaani kwao. Akiwa na miaka 8 aliamua kujiunga na klabu ya JS Suresness. Aliposajiliwa alionekana kioja kwenye timu kwani alionekana mdogo zaidi kuliko wachezaji wenzake wote. Kila mchezaji alimshangaa maana alikuwa na mfupi na alidumaa sana. Wenzake walimcheka maana walidhani hakataweza kucheza dakika 90.

Image result for kante untold story

Ujio wake katika kalbu ile kulileta mabadiliko makubwa sana.

Ugumu wa maisha aliopitia utoto wake ulimfanya pambane na kila aina ya kikwazo. Hatimaye alijizolea jina kubwa zaidi klabuni pale. Kila mtu alianza kumsifia. Mwanzoni alikuwa akiingia kwa dakika 10 za mwisho lakini aliwafundisha wale wenye maumbo makubwa kuwa yeye ni nani. Mwalimu wake anasema alikuwa anacheza kila sehemu ya uwanjani. Alikuwa anacheza kama kichaa. Wakati Fulani mwalimu alimwambia asicheze sana akihofia asije akapata matatizo uwanjani.

Hata timu ilipotwaa kombe alikuwa hana hata muda wa kushangilia maana alijua ile ni sehemu ya kazi.
Image result for kante untold story
ametulia tu pembeni hapo

Wenzake wakiongezeka maumbo yeye alikuwa anabaki pale pale. Alionekana mfupi tokea alipojiunga na klabu hiyo wala hakuonesha dalili ya kwamba kuna namna anaweza kurefuka.

Hilo halikumpa tabu maana alijua anataka kufika wapi.

Image result for kante untold story

Hatimaye baada ya miaka minne akaongezeka kiduchuu. Kutokana na jitihaa zake alijipatia kibarua cha kuwafundisha wachezaji wadogo.

Aliaminika sana na alionekana mtiifu mpole na mchapa kazi. Kisa alijitokeza mtu mmoja ajulikanae kama Pierre Ville ambaye alimua kuchukua majukumu ya kumlea Kante baada ya baba yake kufariki dunia.

Related image

Sehemu ya mwisho nitaimalizia jumatatu. Makala hii imeandaliwa na Privaldinho (Instagram)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here