Home Kimataifa N’golo Kante ajitolea kuchangia kumtafuta Sala

N’golo Kante ajitolea kuchangia kumtafuta Sala

6425
0

Ni siku ya tano sasa imepita na Emiliano Sala hajaonekana. Familia yake imeomba iruhusu watu binafsi waanze mchakato wa kumtafua mpendwa wao.

Serikali ya Ufaransa na Uingereza zilisitisha harakati za kumsaka sala baada ya kuona juhudi zao zinagonga mwamba.

Taarifa zineleza kuwa N’golo amechangia fedha kwa ajili ya kutafuta meli na ndege binafsi ili kuendeleza utaratibu huo wa hapo awali.

Inaeleza wachezaji kadhaa pia wamejitolea kuchangia mchakato huo.

N’Golo Kante yupo tayari kulipia gharama zote ili polisi iendelee na shughuli ya kumtafuta nyota Emiliano Sala aliyepotea kwenye ajali ya ndege.

Klabu ya Leicester City ipo tayari kumrudisha nyota wake anayecheza Fernabache kwa mkopo Brahim Sliman na kumpeleka Cardiff kwa mkopo ili kuwafariji Cardiff baada ya kumpoteza Emiliano Sala

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here