Home Kimataifa NBA Inakuja Afrika Kwa Mara Nyingine Tena, Vikosi Vyatajwa Na Bei Za...

NBA Inakuja Afrika Kwa Mara Nyingine Tena, Vikosi Vyatajwa Na Bei Za Ticket Ni Rafiki.

3193
0

Chama cha mpira wa kikapu nchini Marekani (NBA) na chama cha wachezaji wa mpira wa kikapu nchini Marekani (NBPA) vimetangaza orodha ya wachezaji watakaoshiriki mchezo wa mpira wa kikapu unaousisha wachezaji wa NBA wenye asili ya Afrika na wale wa mabara mengine wanaocheza ligi ya NBA maarufu kwa jina NBA Africa Game. Huu utakuwa mchezo wa pili wa NBA kufanyika Africa na utafanyika siku ya Jumamosi tarehe 5 August kwenye uwanja wa Ticketpro Dome huko Johannesburg, South Africa.  Tickets ambazo zimewekwa kwa bei rafiki kabisa zinapatikana katika website ya ticketpro.co.za.

NBA Africa Game 2017, ambao utafanyika ikiwa ni baada ya hatua/toleo la 15 la mpira wa kikapu bila mipaka yaani  Basketball without Borders (BWB) Africa, kwa mara nyingine itakuwa na mfumo wa Team Africa vs. Team na utachezwa ikiwa pia ni kwa kusaidiana na UNICEF, mfuko wa jamii wa Nelson Mandela (Nelson Mandela Foundation) na SOS Children’s Villages South Africa (SOSCVSA). Kwa wasiofika wataweza kutizama mchezo huu kupitia Kwesé’s TV, inayopatikana kwenye Internet na kwenye application za simu maarufu kama Kwese App.

Kikosi cha Africa, kitakuwa na wachezaji kutoka Africa waliopo NBA na wale ambao wana damu ya Africa lakini wanaishi kwingineko wanaofahamika kama  second-generation African players. Kikosi kitaongozwa na wachezaji wafuatao amba kwenye mabano kuna nchi wanazotokea, asili yao na vilabu wanavyochezea.

Manahodha watakuwa Luol Deng (Los Angeles Lakers; South Sudan) na Thabo Sefolosha (Atlanta Hawks; Switzerland; akiwa na mzazi kutoka South Africa).  Deng na Sefolosha wataungana na wachezaji wengine waliopo kwenye NBA ambao ni.

Bismack Biyombo (Orlando Magic; Democratic Republic of the Congo), Clint Capela (Houston Rockets; Switzerland; wazazi wa  Angola na Congo), Gorgui Dieng (Minnesota Timberwolves; Senegal; zao la BWB Africa 2009), Joel Embiid (Philadelphia 76ers; Cameroon; zao la BWB Africa 2011)*, Serge Ibaka (Toronto Raptors; Congo), Luc Mbah a Moute ( LA Clippers; Cameroon; zao la BWB Africa 2003), Salah Mejri (Dallas Mavericks; Tunisia), Emmanuel Mudiay (Denver Nuggets; Democratic Republic of the Congo), Victor Oladipo (Indiana Pacers; U.S.; mzazi kutoka  Nigeria) and Dennis Schroder (Hawks; Germany; mzazi kutoka  Gambia).

Kwa upande mwingine kikosi cha wachezaji kutoka Mabara mengine kitakuwa kinaongozwa na manahodha Dirk Nowitzki (Mavericks; Germany) na Kemba Walker (Charlotte Hornets; U.S.).

Nowitzki na Walker wataungana na wachezaji wengine ambao ni Leandro Barbosa ( Phoenix Suns; Brazil), Jaylen Brown (Boston Celtics; U.S.), Wilson Chandler (Nuggets; U.S.), DeMarcus Cousins (New Orleans Pelicans; U.S.), Andre Drummond (Detroit Pistons; U.S.), Courtney Lee (New York Knicks; U.S.), Kyle Lowry (Raptors; U.S.), CJ McCollum (Portland Trail Blazers; U.S.) na Kristaps Porzingis (Knicks; Latvia).

Lakini pia watu wengine watakaohusika na mchezo huu ni makochawa NBA watakaoongozwa na Alvin Gentry (Pelicans), Michael Malone (Nuggets) na Erik Spoelstra (Miami Heat),makocha wasaidizi watakuwa David Adelman (Magic), Pat Delany (Hornets), BJ Johnson (Rockets), Sidney Lowe (Washington Wizards), Jamahl Mosley (Mavericks), Patrick Mutombo (Raptors) pamoja na Lloyd Pierce (76ers).

Viongozi kadhaa wa vilabu vya NBA watakuwepo pia na orodha itawahusu kaimu mkurugenzi mtendaji wa Miami Heat Adam Simon, Rais wa Toronto Raptors, Masai Ujiri (Nigeria), na wakufunzi Keith Jones (Rockets)na Ed Lacerte (Celtics), pamoja na waamuzi wa NBA James Capers na Zach Zarba.

 

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here